Agizo la waziri mkuu lafuatwa-Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 27 February 2018

Agizo la waziri mkuu lafuatwa-Bunda Mara





                          Waziri mkuu akiwa mashine ya maji Bunda


                      Mkuu wa wilaya Bunda Mwl.Lydia Bupilipili



Toka amalize ziara yake Waziri Mkuu KASIMU MAJALIWA mwezi January mwaka huu  katika mkoa wa Mara, siku ya majumuisho ya ziara yake Waziri mkuu alitoa  maagizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na agizo la Meneja wa maji Bunda bwana MANSOUR MANDEMLA kukabidhi ofisi na kupisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma mbalimbali zinazoikabili idara hiyo.


Lakini katika hali ambayo ni ya kushangaza kidogo siku ya Jana Februari 26 2018 ndio siku ambayo Meneja huyo amekabidhi rasmi ofisini akiwa chini ya ulizi.

Mapema jana Radio Mazingira ilipata taarifa kuwa Meneja huyo anakabidhi ofisi baada ya kumalizika mwezi sasa toka waziri mkuu atoe agizo hilo.

Baada ya taarifa hizo ikabidi kufika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda ili tuweze kufahamu zaidi kuhusiana na suala hilo maana awali ilisikika kuwa kuna agizo kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mara ikimtaka akabidhi ofisini lakini ikwa kimya tena.

Tulipomuliza Mkuu wa wilaya ya Bunda mwl.LYDIA BUPILIPILI amesema ni kweli Mansour Mandemla amekabidhi ofisi ili apishe uchuguzi na kwamba wameamua kumsimamia kwa ulizi kutokana kuonekana akiwazungusha katika kukabidhiana suala ambalo limewakela kama watendaji wa serikali.

Akiwa katika uwanja wa Sabasaba mjini Bunda KASIMU alisema kuwa  serikali haina nafasi ya kuwavumilia wale wote wanaoharibu miradi ambayo serikali imetoa pesa ili kuwasaidia wananchi wake hivyo kabla wananchi hawajapata madhara mtu huyo au watu hao wataondolewa mara moja kwani inaonekana wazi wameshindwa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuwatumikia wananchi

No comments:

Post a Comment