Penati alizokosa Chirwa ndani ya miezi miwili - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 10 February 2018

Penati alizokosa Chirwa ndani ya miezi miwili


Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa amekosa mkwaju wa tatu wa penati kati ya tano ambazo amepiga katika kipindi cha miezi miwili (Januari na Februari).
Penati ambayo amekosa leo kwenye mchezo wa kimataifa kati ya Yanga dhidi ya St. Louis ndiyo ilikuwa ya tatu kukosa kati ya tano alizopiga. Yanga ilipata penati dakika ya 24 katika mchezo baada ya Hassan Kessy kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari.
10/01/2018 Alikosa mkwaju wa penati kwenye mechi ya nusu fainali ya Mapinduzi Cup Yanga vs URA.
30/01/2018 Akafunga mkwaju wa penati dhidi ya Ihefu FC kwenye michuano ya FA Cup ndani ya dakika 90.
30/01/2018 Alikosa penati ya pili wakati wa kuamua mshindi wa mchezo wa FA Cup vs Ihefu.
06/02/2018 Alifunga mkwaju wa penati kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara vs Njombe Mji.
10/02/2018 Amekosa penati ya tatu vs St. Louis mchezo wa Caf Champions League.

No comments:

Post a Comment