Waziri mkuu wa Korea kusini Lee
Nak-yeon amebaini wazi kwamba kuna masharti ambayo lazima yabainishwe kabla ya
kukubali mwaliko wa uongozi wa nchi hiyo kukutana na kiongozi wa Korea
kaskazini, Kim Jong-un.
Jana katika hatua kubwa ya
kidiplomasia kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alimwalika mwenzake wa
kusini kwa mkutano lakini Rais Moon Jae-in bado hajatoa jibu la kuitikia wito
huo au la.
Ujumbe huo umetolewa na dada yake
kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un ambaye aliandamana na maafisa wa ngazi
za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea Kusini tangu kumalizika kwa
vita vya Korea miaka 60 iliyopita.
Hata hivyo hatua hiyo haijafurahiwa
na Marekani ambayo ingali inataka kwanza Korea kaskazini ishinikizwe kuachana
na miradi yake ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment