Mwananchi ajitolea eneo la ujenzi wa zahanati-Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 20 February 2018

Mwananchi ajitolea eneo la ujenzi wa zahanati-Bunda Mara

Wananchi wakiwa wamekaa katika mkutano wa hadhara siku ya jana eneo la rubana shule ya msingi kata ya Balili  


MANYANKI MARWA MAMBA mkazi wa Kata ya Balili Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani amejitolea eneo lenye urefu wa hatua 50 na upana wa hatua 30 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Amesema ameguswa na Maendeleo katika Kata hiyo kwani wameteseka kwa muda mrefu kwa kukosa huduma ya Afya. 

Bwana MAMBA amesema pamoja na kukosa huduma pia amefanya hivyo baada ya uongozi kutafuta eneo la kujenga zahanati kwa muda mrefu bila mafanikio. 

Naye kwa upande wake Elizabeth Anania mkazi wa Balili amesema wanateseka kwa kukosa huduma ya afya hasa wajawazito. 

Amesema serikali wakianza utaratibu wa ujenzi wa zahanati hiyo watachangia shuguli za maendeleo Kama kusogeza mawe, michanga na kokoto. 

Hata hivyo Diwani wa Kata hiyo THOMAS TAMKA amesema kwamba ujenzi wa zahanati hiyo umepata ufadhili wa TANAPA baada ya kikao kilichofanyika mwaka Jana baina yao na wananchi kwa ajili ya kuimarisha ujirani mwema.

No comments:

Post a Comment