Kilimahewa waomba wajengewe tenki la maji-Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 27 February 2018

Kilimahewa waomba wajengewe tenki la maji-Bunda MaraWakazi wa mtaa wa Kilimahewa kata ya Kabalimu Halmashauri ya mji wa Bunda wameiomba serikali kujenga tenki la maji katika vilima vya Kilimahewa ili kutatua tatizo la maji katika mtaa huo wenye wakazi 2000.

Ombi hilo limetolewa na mdau wa maji bwana MUSA MADUKA alipokuwa akizungumza na radio mazingira fm leo kutokana na uhaba mkubwa wa maji unaowakumba wananchi hao.

MUSA MADUKA amesema kuwa kutokana na taarifa yake aliyoiwasilisha idara ya maji ya mji wa bunda ameiomba serikali kuifanyia kazi ili kuwapunguzia wanawake wa mtaa huo kutembea umbali mrefu ili kutafuta maji.

Mkazi wa mtaa huo SIMON BALOLAGE amesema kuwa ni vizuri serikali ikaharakisha kujenga tanki hilo ili kuwarahisishia wananchi hao upatikanaji wa maji safi na salama.

Kwa upande wake mdau wa maji mji wa Bunda SULEIMAN NASSORO ameeleza kuwa kuna mpango wa kujenga tenki la maji katika vilima vya kilimahewa ili kuongeza nguvu ya maji ili kutatua kero ya maji.

No comments:

Post a Comment