Mkuu wa Shule ashushwa cheo kupisha uchunguzi -Bunda Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 28 February 2018

Mkuu wa Shule ashushwa cheo kupisha uchunguzi -Bunda MaraSiku chache baada ya redio mazingira fm, kuripoti habari inayoeza kuwa mwalimu mkuu katika shule ya sekondari Nansimo kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha zilizochangwa na wananchi hatimae mwalimu huyo ameshushwa wadhifa wake na kuwa mwalimu wa kawaida.

Akizungumza na kituo hiki leo mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Costantini Mizani  amethibitisha kutokea hilo na kueleza kuwa hatua hiyo imekujia baada ujio wa kaimu afisa elimu wilaya pamoja na afisa elimu taaluma kufika shuleni hapo kufutilia suala hilo.

Amesema mwalimu huyo meshushwa cheo kupisha uchunguzi na kwamba tayari amesharipoti mwalimu mwengine kuchukuwa nafasi yake.

No comments:

Post a Comment