STAA wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kumtia
matatani askari magereza mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja,
Ijumaa Wikienda lilishuhudia mkanda mzima.
Ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Kitengo cha Ustawi wa
Jamii, askari huyo alisahau kofia yake ya kazi yenye Krauni ya Bibi na
Bwana kwenye kiti aina ya ‘benchi’ ambapo Diamond alipofika aliikalia,
jambo ambalo ilielezwa kuwa si sawa kwa sheria za kiaskari.
Ijumaa Wikienda lilimshuhudia askari huyo akinyanyuka haraka kwenye
benchi hilo kisha kumpisha Diamond na mwanasheria wake ambao walikaa na
kuendelea na mazungumzo yao wakati mlinzi wa msanii huyo, Mwarabu
Fighter akichukua sendoz za Diamond zilizokuwa zimekatika na kwenda
kuzishona.
Wakati Mwarabu akichukua sendoz hizo, Diamond alishuhudiwa akirudi nyuma
na kuikalia kofia hiyo yote bila kujua huku askari huyo akihaha
kuitafuta kofia hiyo.
Hata hivyo, askari huyo alikuja kuiona na kofia hiyo baada ya Diamond
kusimama, jambo ambalo liliwasababisha askari wenzake akiwemo mkuu wao
kumuita na kumuonya mwenzao kuwa alikuwa amefanya kosa kubwa la kisheria
za kipolisi.
Ijumaa Wikienda lilipotaka kujua kosa alilolifanya askari huyo
lilimuuliza mmoja wa maafisa hao ambaye hakutaka kutajwa kwa kuwa siyo
msemaji wa jeshi hilo ambapo alisema kuwa, kofia za askari ni sehemu ya
sare na ni kosa kubwa kutoka mwilini mwa askari na kuchezewa kwa kujua
au kutojua na raia wa kawaida.
“Kimaadili ya kazi ni sawa na bunduki ndiyo maana kijeshi ukiona askari
amevuliwa kofia na mkuu wake, ujue huo ndiyo mwisho wa kazi yake. Maana
yake anakuwa amepoteza sifa za kulitumikia jeshi.
“Huyo askari amshukuru Mungu kwa kupewa tu onyo, lakini angeweza
kupoteza kabisa sifa ya kulitumikia jeshi la magereza,” alisema mmoja wa
maafisa wa jeshi la magereza aliyeeonekana kuwa na cheo kikubwa tofauti
na wengine.
Monday 12 February 2018
Diamond amtia matatani Askari Magereza
Tags
# BURUDANI
Share This
About mazingirafm
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment