Hospital ya Manyamanyama imepokea vifaa venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nane viliyotolewa na Rais wa Tanzania - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 27 February 2018

Hospital ya Manyamanyama imepokea vifaa venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nane viliyotolewa na Rais wa Tanzania




                             
Baadhi ya vitanda vilivyotolewa
Hospitali  ya  Manyamanyama  iliyopo  katika halmashauri  ya mji  wa  Bunda   mkoani  Mara  jana  jumatatu imepokea  vitanda ,magodoro pamoja na  mashuka yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nane viliyotolewa na Rais wa Tanzania kupitia wizara ya afya na kukabidhiwa hospitalini hapo na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Agness Marwa.


Akizungumza wakati wa kukabidhi  vitanda  hivyo  mbunge  wa viti maalum mkoa wa Mara  kupitia tiketi ya CCM Agness Marwa ambae pia amekuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo amesema kuwa anamshukuru  sana Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John  Pombe Magufuri kwakutoa vifaa hivyo kupitia wizara ya afya hivyo kufanya huduma katika hospitali za serikali kuendelea kuwa bora zaidi.

Bi.Agness amekabidhi  hospitalini hapo vitanda  vya kawaida  ishirini,vitanda vya kuzalia vitano,magodoro ishirini na mashuka hamsini  vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nane ambapo amesema kuwa tayari serikali imetoa milioni mia tano kwa ajiri ya ukarabati wa majengo  hospitalini hapo kwa lengo la kuokoa vifo vya wakinamama na watoto.

Naye mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Bunda dr.Nikodemasi nikorausi Masosota amempongeza raisi  Magufuri kwa kuyaona  matatizo ya watanzania hasa wakinamama na watoto  ambao walikuwa wanalala chini hivyo kuona  umuhimu wa kusambaza vitanda kwa kila halmashauri hapa nchini kwani idara ya afya imekuwa nachangamoto nyingi  nchini .

No comments:

Post a Comment