Wakazi wa kijiji cha
Nansimo katika halmashauri ya wilaya ya bunda mkoani Mara wamemkataa Mwalimu
mkuu wa shule ya sekondari Nansimo kwa madai ya kutafuna fedha za michango ya
wazazi waliyotoa kwaajili ya kulipa waalimu wa kujitolea.
Wakizungumza katika mkutano
wa shule na wazazi kilichoketi shuleni hapo wazazi hao wameonyesha
kutoridhishwa na namna fedha walizochanga zinavyotumika kuwalipa walimu hao
huku wakieleza kwamba taarifa wanazopewa ya malipo ya walimu ni tofauti na hali
halisi.
Akitoa ufafanuzi wa
madai hayo Mwalimu mkuu wa shule hiyo elias Supira ameeleza kwamba taarifa
walizo nazo wazai ni batili kwakuwa walimu hao wanalipwa kwa kufuata utaratibu
uliowekwa kwa mujibu wa mkataba.
Naye mwenyekiti wa
kamati ya maendeleo ya kata ambae pia ni diwani wa kata hiyo bwana sabato
mafwimbo amesema kwamba anaheshimu mawazo ya wananchi lakini mwenye maamuzi ya
kumuhamisha mwalimu ni mkurugenzi wa halmashauri.
No comments:
Post a Comment