Halmashauri ya mji wa Bunda yapeleka walimu 43 shule ya Msingi. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 19 February 2018

Halmashauri ya mji wa Bunda yapeleka walimu 43 shule ya Msingi.


Imeelezwa kuwa Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara imeshakamilisha utaratibu wote wa maelekezo yaliyotolewa na  serikali kuhusu kuwapeleka  wale walimu wa ziada kutoka shule za sekondari kwenda shule za msingi. 

Akizungumza na Mazingira Fm mwishoni Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya mji wa Bunda Mtundi Nyamhanga ofisini kwake amesema Walimu 43 ndio waziada ndani ya Halmashauri na kwamba wote 43 wameshapangiwa vituo vya kazi kama ilivyoelekezwa.

Nyamhanga amesema wapo baadhi ya walimu kipindi maelekezo yanatoka waliomba wenyewe wapelekwe msingi na wapo wengine baadhi waliomba wasipelekwe msingi huku wakitoa sababu za kwanini wasipelekwe huko.

Pamoja na hayo Mtundi amesema wao kama ofisi walizingatie maelekezo ya serikali kama ilivyoelekezwa na sio vinginevyo.No comments:

Post a Comment