Huduma ya Afya bado kitendawili mkoani Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 26 February 2018

Huduma ya Afya bado kitendawili mkoani MaraSerikali mkoani Mara imekiri kukabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi katika hospitali ya rufaa ya Musoma kufuatia kuwapo kwa ongezeko la wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu hospitalini hapo hali inayorejesha nyuma azma ya serikali katika uboreshaji wa huduma ya afya nchini.

Akizindua duka la dawa la hospitali ya rufaa ya Musoma mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima amesema licha ya serikali kuonesha nia ya kupanua huduma za afya lakini bado maeneo mengi yanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wahudumu kufuatia ongezeko la wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabau hospitalini hapo.

Aidha Malima ameongeza kuwa kuzinduliwa kwa duka la madawa hospitalini hapo si tu kutasaidia kupunguza kero kwa wagonjwa kununua madawa maeneo ya mbali lakini pia itasaidia kuongeza mapato ya serikali.

No comments:

Post a Comment