Huyu ndiyo chura wa aina yake anayetafutiwa mchumba - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 10 February 2018

Huyu ndiyo chura wa aina yake anayetafutiwa mchumba

Chura kutoka kizazi kisicho cha kawaida anatafutiwa mke Bolivia

Wataalam wa kuhifadhi wanyama nchini Bolivia wameanza kutembea taifa zima wakimsaka chura wa 'kike' atakayejamiana na chura mmoja asiye wa kawaida ambaye wanahofia kizazi chake huenda kikaangamia.

Chura huyo aliyepewa jina la 'Romeo' na aliye na mwenye umri wa miaka 10, anaishi katika maji na amekuwa akimtafuta mwenzake kwa kipindi cha miaka tisa.

Tayari amewekwa katika mtandao wa kuwakutanisha wapendanao akisema : Namtafuta mpenzi juliet.

Wanasayansi kwa sasa wanatufa katika vidimbwi vya maji mbali na mito kwa chura wa kike ambaye atajamiana na chura huyo ili kuhifadhi kizazi hicho.

''Hatutaki yeye apoteze matumaini. lakini wahifadhi hao watalazimika kuongeza kasi ya kumsaka chura huyo wa kike kwa kuwa hawezi kuishi zaidi ya miaka 15''.

Hiyo inaamaanisha kuwa Romeo anayeishi katika pipa katika kumbukumbu ya Cochabamba amesalia na miaka mitano kuishi ili kuhifafhi kizazi chakeHizi ni miongoni mwa harakati za wanasayansi kumtafutia mchumba

Ikiwa ni kati ya kampeni ya kuchangisha $15,000, kabla ya siku ya wapendanao ya Valentine, mtandao huo wa kuwakutanisha wapendanao uliweka jina la Romeo pamoja na picha yake mbali na ujumbe unaomuhusu.

''Namtafuta Juliet wangu kwa sababu mimi ni kizazi cha mwisho cha familia yangu''.

''Namtufuta chura wa kizazi changu, la sivyo kizazi changu chote kitaangamia''.

Chanzo-  BBC

No comments:

Post a Comment