Wednesday, 28 February 2018

Mkuu wa Shule ashushwa cheo kupisha uchunguzi -Bunda Mara



Siku chache baada ya redio mazingira fm, kuripoti habari inayoeza kuwa mwalimu mkuu katika shule ya sekondari Nansimo kuhusishwa na ubadhirifu wa fedha zilizochangwa na wananchi hatimae mwalimu huyo ameshushwa wadhifa wake na kuwa mwalimu wa kawaida.

Akizungumza na kituo hiki leo mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Costantini Mizani  amethibitisha kutokea hilo na kueleza kuwa hatua hiyo imekujia baada ujio wa kaimu afisa elimu wilaya pamoja na afisa elimu taaluma kufika shuleni hapo kufutilia suala hilo.

Amesema mwalimu huyo meshushwa cheo kupisha uchunguzi na kwamba tayari amesharipoti mwalimu mwengine kuchukuwa nafasi yake.

Angalia Nyimbo 13 za Bongofleva ambazo TCRA imeagiza zisipigwe Redioni wala TV

    chanzo Ayo tv                 

Bupilipili awaongoza UVCCM Wilaya ya Bunda katika ushiriki wa ujenzi wa kituo cha Afya Bunda



Umoja vijana wa chama cha mapinduzi uvccm wilaya ya Bunda mkoani Mara chini ya mwenyekiti wake gasper Charles wameshiriki kutoa msaada wa kusaidia ujenzi katika kituo cha afya bunda kinacho jengwa katika kata ya Kabarimu.

Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la ujenzi wa kituo hicho cha afya Bwana Gasper amesema kuwa katika kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi wameamu kuungana na viongozi wa chama hicho katika ujenzi huo kwa maslahi mapana ya wananchi pamoja na kumsaidia rais john pombe magufuli kusimamia miradi ya maendeleo inayoendelea nchini.

Naye katibu wa umoja huo shija steven amewaomba vijana mjini bunda kutumia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kujipatia ajira badala ya kukaa vijiweni bila kazi.

Hata hivyo katika kusaidia ujenzi wa kituo hicho mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda ambae pia ni mkuu wa wilaya Mwl. Lydia Bupilipili ameshirikiana na vijana hao katika kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho kilichotolewa fhedha shilingimilioni mia tano inakamilika kwa ufanisi wa hali ya juu , pia amewapongeza vijana wa umoja wa chama hicho katika kuonyesha uzalendo wa kweli.

Tuesday, 27 February 2018

Angalia Video mpya ya Chege Ft.Saida Karoli - Kaitaba

                    

Alichokibaini Naibu Waziri Mavunde katika ziara ya kushtukiza Mwanza

chanzo ni AYO TV

Agizo la waziri mkuu lafuatwa-Bunda Mara





                          Waziri mkuu akiwa mashine ya maji Bunda


                      Mkuu wa wilaya Bunda Mwl.Lydia Bupilipili



Toka amalize ziara yake Waziri Mkuu KASIMU MAJALIWA mwezi January mwaka huu  katika mkoa wa Mara, siku ya majumuisho ya ziara yake Waziri mkuu alitoa  maagizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na agizo la Meneja wa maji Bunda bwana MANSOUR MANDEMLA kukabidhi ofisi na kupisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma mbalimbali zinazoikabili idara hiyo.


Lakini katika hali ambayo ni ya kushangaza kidogo siku ya Jana Februari 26 2018 ndio siku ambayo Meneja huyo amekabidhi rasmi ofisini akiwa chini ya ulizi.

Mapema jana Radio Mazingira ilipata taarifa kuwa Meneja huyo anakabidhi ofisi baada ya kumalizika mwezi sasa toka waziri mkuu atoe agizo hilo.

Baada ya taarifa hizo ikabidi kufika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda ili tuweze kufahamu zaidi kuhusiana na suala hilo maana awali ilisikika kuwa kuna agizo kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mara ikimtaka akabidhi ofisini lakini ikwa kimya tena.

Tulipomuliza Mkuu wa wilaya ya Bunda mwl.LYDIA BUPILIPILI amesema ni kweli Mansour Mandemla amekabidhi ofisi ili apishe uchuguzi na kwamba wameamua kumsimamia kwa ulizi kutokana kuonekana akiwazungusha katika kukabidhiana suala ambalo limewakela kama watendaji wa serikali.

Akiwa katika uwanja wa Sabasaba mjini Bunda KASIMU alisema kuwa  serikali haina nafasi ya kuwavumilia wale wote wanaoharibu miradi ambayo serikali imetoa pesa ili kuwasaidia wananchi wake hivyo kabla wananchi hawajapata madhara mtu huyo au watu hao wataondolewa mara moja kwani inaonekana wazi wameshindwa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuwatumikia wananchi