Wazazi Wilayani Bunda watakiwa kula sahani moja na watoto wao waliohitimu kidato cha nne hadi matokeo yatoke - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 24 December 2017

Wazazi Wilayani Bunda watakiwa kula sahani moja na watoto wao waliohitimu kidato cha nne hadi matokeo yatoke

Baada ya wanafunzi wa kidato cha nne kote  nchini  kumaliza mtihani wao mnamo mwezi wa 11   mwaka huu, wazazi na walezi wa watoto hao wametakiwa kuendelea na ushirikiano ule ule wa kuwalea watoto hao katika maadili mema.

Hayo yamesemwa na  baadhi ya wakazi wa kata ya kabarimu  halmashauri ya mji wa bunda kwa nyakati tofauti ambapo wamesema kuwa wapo baadhi ya wazazi hujisahau kuwapa malezi mazuri watoto hao na kuwaacha wakifanya mambo yasiyo yakimaadili kama kujihusisha na vitendo vya ngono.


Mmoja wa wakazi hao bwana Thomas Ezekil amesema kuwa wazazi wanapaswa kutambua kwamba watoto hao bado ni wanafunzi na wanasubiri matokeo yao ili waendelee na masoma yao.

No comments:

Post a Comment