vitendo vya ubakaji katika Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoni Mara bado vinaendelea kushika kasi - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 20 December 2017

vitendo vya ubakaji katika Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoni Mara bado vinaendelea kushika kasi

vitendo vya ubakaji katika Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoni Mara bado vinaendelea kushika kasi baada ya baba mmoja mwenye umri wa miaka 37 kuripotiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili katika kata ya nyamakokoto.
Akizungumza mtoto huyo jina tunalihifadhi amesema kuwa alikuwa akishawishiwa na baba huyo kwa kumpa hela, huku akikataa na hatimae siku moja akenda kuoga bafuni akamfanyia tendo hilo la ubakaji na kumweleza kuwa asitoe taarifa kwa wazazi wake kwani akifanya hivyo atamnyonga.
Aidha mama wa mtoto ameeleza kwamba alimuona mwanae akitembea akiwa ameachanisha miguu na kumuuliza ambapo mtoto huyo alimkimbia mama yake, hivyo alilazimika kumshawishi na kumweleza kwamba alibakwa na baba huyo.
Aidha baada ya kutoa taarifa polisi aliambiwa ampeleke mtoto hospitali kwa vipimo na kuonyesha kuwa ni kweli mtoto huyo amefanyiwa kitendo hicho.

Taarifa zilizopo ni kwamba alikamatwa na polisi mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment