Wananchi wa
kijiji cha Ruamkoma kata ya Butiama
Wilaya ya Butiama mkoani Mara wameiomba serikali kuwaboreshea miundombinu
ya barabara katika kijiji hicho kwani wamekuwa wakishidwa kufanya shughuli za
kimaendeleo katika kijiji hicho.
Hayo
yamesemwa na wananchi wa kijiji wa ruamkoma wakati wakizungumza na mazingira fm
kwa nyakati tofauti.
Mwikwabe
Marwa ambae ni miongoni mwa wananchi hoa amesema kuwa wamekuwa wakipata shida
kubwa ya kusafirisha bidhaa zao za biashara kutokana na ubovu wa barabara
zilizopo katika kata hiyo na kuwalazimu kutumia gharama kubwa wakati wanapokuwa
wanasafirisha bidhaa zao.
Aidha
wamesema changamoto zingine wanazokumbana nazo ni pamoja na maji, umeme, na
upungufu wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi na kuomba serikali
kuwapelekea huduma hizo.
No comments:
Post a Comment