Pesa ya mahindi ya msaada yamludisha Mstaafu ofisini kujibu wilayani Bunda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Monday 4 December 2017

Pesa ya mahindi ya msaada yamludisha Mstaafu ofisini kujibu wilayani BundaBaraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara limetoa siku tano kuanzia leo kwa aliyekuwa afisa kilimo ambaye kwa sasa amestaafu kuhakikisha anatoa taarifa ya kujitosheleza kuhusu uchakachuaji uliofanyika katika pesa ya mahindi ya msaada yalioyogawika ndani ya  halmashauri.

Azimio hilo limetolewa leo katika kikao cha dharura cha kujadili hoja ya mkaguzi wa ndani kutoka mkoani ambapo hoja hiyo emepelekea hadi  kuimbua mambo mengine yaliyokuwa yamejificha ndani.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri Isack Mahela amesema wao kama wawakilishi wa wananchi hawawezi kukaa kimya wakati pesa za wananchi zinatumika sivyo.

Hata hivyo inaelezwa kuwa anayetuhumiwa kuhusuiana na suala hilo la pesa ya mahindi ya msaada kupotea juu juu  afisa huyo ameshasitaafu hivi karibuni.

Awali madiwani wameonekana kutolizishwa na majibu ya wakuu wa idara katika mambo ya msingi yanayohusu halmashauri jambo ambalo wamesema kwa hali hiyo wataisababishia halmashauri hati mbaya.

No comments:

Post a Comment