Taasisi za
serikali pamoja na taasisi Binafsi katika Wilaya ya Bunda Mkoani Mara wametakiwa
kusimamia ipasavyo suala la pembejeo zinazotakiwa kuwafikia wa wakulima ili kuwawezesha
kulima kilimo bora na sio bora kilimo.
Agizo hilo
limetolewa Jana na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwalimu Lydia Bupilipili wakati akifungua
wa mdahalo kuhusu Pembejeo feki Wilayani Bunda ulioandaliwa na Baraza la kilimo
na mifugo Tanzania |Agricultural Council of Tanzania ] katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Bupilipili
amesema Taasisi zinazohusika na usimamizi wa pembejeo wasipokuwa makini siku
zote wataendelea kutiwa doa na wale wasiowatakia meme katika kazi yao hivyo
amewataka kuamka nakuona sasa si muda wakufumbia macho masuala kama hayo.
Bupilipili
amesema Wilaya ya Bunda inaongoza kwa pembejeo feki hivyo kuna kila sababu ya kuwa
makini na watu wasio takia mema taifa lao kupitia kusambaza pembejeo feki kwa
wakulima.
Bwana Khalid
Ngassa kutoka Baraza La kilimo na mifugo Tanzania kwa upande wake amesema kuwa
wakulima wanapata hasara kubwa na wanaumia sana kupitia pembejeo feki
wanazopokea kutoka kwa wasambazaji hali ambayop inapelekea wakulima kukata tamaa
na kilimo hivyo ameshauri wakulima nao wawe makini na pembejeo hizo ikiwa ni
pamoja na kutoa taarifa mapema kama wakigundua kunadosari popote.
Kwa upande
wao wakulima wa Wilaya Bunda wamekubalia kwa kauli moja ya kufuata ushauri
waliopewa ikiwa ni pamoja na kusema pale ambapo kuna kasoro ili wawahi
kusaidiwa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment