Mayanja asema na Wanawake wa mji wa Bunda kuhusu kujiunga katika SACCOS - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday 29 December 2017

Mayanja asema na Wanawake wa mji wa Bunda kuhusu kujiunga katika SACCOSMkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda Janeth Mayanja amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa saccos ya wanawake itakayozinduliwa mnamo january 4 2018 katika viwanja vya halmashauri hiyo.

Akizungumza na redio mazingira fm, Mayanja amesema kuwa siku hiyo ya uzinduzi wataanza kwa maandamano yakayoanzi  benki ya NMB mpaka viwanja vya halmashauri ya mji wa bunda.

Aidha amesema halmashauri kwa kugundua kilio na uhitaji wa wanawake katika mji wa bunda waliamua kuunda saccos hiyo itakayowasaidia wanawake kuinuka kiuchumi.

Hata hivyo amewataka wanaume kuwaunga mkono wanawake ili kufanikisha uchumi wa pamoja.

No comments:

Post a Comment