Wasifu wa Kituo
Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kituo kinarusha matangazo yake kutoka Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani, ikiwemo Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza kama Magu na Ukerewe.
Kupitia vipindi na matangazo yake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.

No comments:
Post a Comment