Imeelezwa
kuwa ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni katika Mtaa wa Sabasaba Kata ya
Bunda Mjini Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara na kusababisha kuungua kwa
maduka mawili inasadikika kuwa chanzo cha ajali hiyo ni shoti ya umeme.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusu tukio hilo Mkuu wa kituo cha polisi wilaya
ya Bunda OCD Jeremiah
Shila amesema kuwa kwa uchungzi wa awali wakishirikiana
na Tanesco wameweza kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni shoti ya umeme
iliyojitokeza katika moja ya maduka yaliyoungua.
Shila
amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi zaidi ili waweze kubaini kisa kamili
cha ajali hiyo.
Aidha
Shila amesema kwa ushirikiano mzuri wa wananchi pamoja na Jeshi la polisi
waliweza kuuzima moto huo licha ya kuwepo kwa changamoto ya gari la zima moto
katika Wilaya Bunda.
Hata
hivyo Shila ametoa wito kwa Wananchi wa wilaya ya Bunda kuwa wangalifu na umeme
ikiwa ni pamoja na kuacha kupikia kwenye vibanda.
Ajali
ya moto ilitokea mnamo tarehe 18.12.2017 majira ya saa tatu usiku katika mtaa
wa sabasaba maeneo ya maduka ya wauza mitumba karibu na mlango wa kuingia soko
kuu la mjini Bunda.
No comments:
Post a Comment