Bodi ya filamu tanzania yatuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha muigizaji nguli wa filamu shamila mfikirwa. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 21 October 2017

Bodi ya filamu tanzania yatuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha muigizaji nguli wa filamu shamila mfikirwa.

Bodi ya Filamu Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Muigizaji nguli Shamila Mfikirwa.
Katika Salamu zake kwa Rais ya Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifamba, Mwenyekiti wa chama cha Waigizaji Ndugu Elia Mjata na wanafamilia wa filamu na uigizaji kwa ujumla Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.
“Kwa niaba ya Bodi nachukua fursa hii kutoa pole nyingi sana kwa familia ya marehemu kutokana na kuondokewa na mpendwa wao, pia Bodi imeguswa na msiba huo na inawaombea wanafamilia kwa Mungu kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu” alisema Bi.Fissoo.
Mwigizaji Shamila Mfikirwa maarufu kama ‘Shamila’ amefariki dunia katika Hospitali ya Occean Road Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2017 alipokuwa akipatiwa matibabu.
Innalilah Wainna Ilayhi Rajiun.
Imetolewa na

Bodi ya Filamu Tanzania.

No comments:

Post a Comment