Siku chache baada ya kituo hiki kuripoti habari kuhusu mifugo zaidi ya 700
kufa kwa tatizo la kukosa maji na majani kwa muda mrefu, hatimae leo mkuu wa
idara ya mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa bunda Mkoani Mara bwana Rick
steven Kaduri amejitokeza na kupinga ukweli wa taarifa hiyo licha ya kukiri
kuwa mifugo imekufa.
Amesema kuwa ni kweli mifugo imekufa katika
halmashauri ya mji wa bunda, lakini ameshangazwa na idadi iliyotajwa ya mifugo
zaidi ya 700 kufa huku akisema kuwa kwa
taarifa walizonazo kama halmashauri nzima ni zaidi ya mifugo 1000 imekufa kwa
kukoswa maji na majani kwa muda mrefu.
Amesema taarifa kama hizo zilisikika tena guta kuwa
zaidi ya ng’ombe 3000 wamekufa lakini bado wanazidi kuzifanyia uchunguzi
kubaini ukweli wake.
Amesema tatizo la mifugo kufa imetokana na ukame wa
muda mrefu huku akitaja kuwa wafugaji waliokuwa na ng’ombe wenge ndio
waathirika wakubwa hivyo amewakumbusha wafugaji kufuga kisasa ili waweza kumudu
hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hivi karibuni mtandao huu umewatembelea wafugaji wa
kijiji na kata ya rwabu kutaka kujua hali ya mifugo ambapo mwenyekiti wa kijiji
hicho bwana Gelad Kuzenza, alisema kuwa kwa makisio ya chini walikuwa na
ng’ombe 1500 na lakini kwa sasa wamebaki
700 huku akieleza kuwa bei ya ng’ombe imeshuka hadi shilingi 15,000 huku
wanunuzi wakisusia kununua mifugo hiyo wakati mwingine kutokana na hali ya ya
kudhoofika zaidi.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha
wafugaji kanda ya ziwa kwa maana ya mikoa ya Mara, simiyu shinyanga, mwanza geita na Kagera
bwana Mrida mshota amekiri kuwepo kwa tatizo la mifugo mingi kufa kwa ukame na
hasa ng’ombe ambapo amesema kuwa wameshaanza mikakati ya kukabiliana na tatizo
hilo kwa kuanzisha mashamba ya majani kwa ajili ya mifugo yao.
Amesema zoezi hilo sio la muda mfupi kwa kuwa
watanzania wengi na hasa mikoa ya kanda ya ziwa bado wanafuga ng’ombe wa
kienyeji na wana mifugo mingi.
Amewataka wafugaji kuanza kubadilika kwa kufuga
kisasa ili waweze kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
No comments:
Post a Comment