Jumla ya
wazee 235 katika kata ya neruma wilayani Bunda Mkoani Mara wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa
matibabu lengo ikiwa ni kuhakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa fursa ya
kushiriki katika mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku.
Akisoma taarifa
ya utoaji wa huduma za afya na stawi wa jamii Kwa mgeni Rasmi Kaimu Afisa
Ustawi wa Jamii wilaya ya bunda Liberatus Kazana katika maadhimisho ya siku ya
wazee Duniani yaliyofanyika Katika kijiji cha Neruma kata ya neruma Oktoba 20
amesema Halmashauri ya wilaya ya Bunda inajumla ya wazee 9,994 waliona miaka 60
na kuendelea.
Kazana
Amesema kunachangamoto mbalimbali katika uendeshaji wa huduma za afya na hasa
katika kuwahudumia wazee huku gharama za uendeshaji wa huduma za msamaha
zimekuwa kubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya hiyo ikitokana na idadi
kubwa ya wagonjwa wanaohitaji msamaha kama vile akina mama wajawazito,watoto
chini ya miaka mitano,walemavu na wazee.
Kwa upande
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya ya Bunda
Masalu Kisasira amesema wao kama serikali wanatambua changamoto hizo hivyo
ameahidi kuzifanyia kazi huku akiwasihi wazee kuwa kioo kizuri kwa watoto wao
kwa kuwaonya na kuwashauri ili kuwawezesha watoto wao kuwa na misingi bora ya
maisha.
xczxvzcxvc
ReplyDelete