← NYUMBANI
MAZINGIRA FM • BUNDA, MARA

Wasiliana Nasi

Kwa habari, matangazo, udhamini, ushirikiano na mawasiliano ya jumla.

SIMU+255 621 046 491 PIGA SIMU →
BARUA PEPEmazingirafm@gmail.com TUMA BARUA →
ANWANIP.O. Box 51, Saranga/Kabarimu

Bunda, Mara • 31530

MATANGAZO NA UDHAMINI

Fanya kazi na Mazingira FM

Kwa matangazo ya biashara, udhamini wa vipindi, kampeni za jamii na ushirikiano wa mawasiliano, wasiliana nasi kupitia simu au barua pepe.

TUFUATE

Mazingira FM Mitandaoni

Facebook Instagram YouTube X / Twitter
← NYUMBANI
MAZINGIRA FM • 91.7

Kuhusu Mazingira FM

Sauti ya Jamii — redio yenye maudhui ya kijamii kutoka Bunda, Mkoa wa Mara.

Wasifu wa Kituo

Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kituo kinarusha matangazo yake kutoka Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani, ikiwemo Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza kama Magu na Ukerewe.

Kupitia vipindi na matangazo yake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.

MTANDAO WETU

Vituo Vinne vya Matangazo

BUNDAKituo Kikuu
MUSOMAMara
TARIMEMara
MUGUMU–SERENGETIMara
SAUTI YA JAMII

Redio ya Jamii

Mazingira FM inalenga kuipa jamii nafasi ya kupata habari na maarifa, kusikiliza mijadala yenye manufaa, kushiriki katika masuala yanayoigusa na kupata burudani kupitia vipindi vinavyoakisi maisha ya jamii.

← NYUMBANI
MAZINGIRA TV

Video kutoka Mazingira FM

Tazama habari, mahojiano, matukio ya jamii na vipindi vya Mazingira FM.

MAZINGIRA FM • VIDEO

Mazingira TV

Video za habari na shughuli za jamii kutoka Bunda, Mara na maeneo yanayofikiwa na Mazingira FM.

FUNGUA YOUTUBE →
MAZINGIRA FM 91.7
Sauti ya Jamii • Mara, Tanzania
← NYUMBANI
MAZINGIRA FM NEWSROOM

HABARI

Habari na taarifa kutoka Mazingira FM.
Inapakia habari...
▶ SIKILIZA LIVE
← RUDI HABARI MPYA
Inapakia habari...
MAZINGIRA FM • Sauti ya Jamii • Mara, Tanzania
HABARI MPYAMazingira FM • Sauti ya Jamii • Habari kutoka Mara
MAZINGIRA FM • MARA

Mazingira FM.
Sauti ya Jamii.

Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kituo kinarusha matangazo yake kutoka Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani, Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza kama Magu na Ukerewe. Kupitia vipindi na matangazo yake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.

SOMA HABARI
Mtandao wetu

Vituo 4 vya Matangazo

BundaMain Site
MusomaTransmission Site
TarimeTransmission Site
MugumuSerengeti
Newsroom

Habari Mpya

Machapisho mapya kutoka Mazingira FM.

HABARI ZA SASA
Inapakia habari mpya kutoka Radio TADIO...
HABARI ZAIDIHabari kutoka kwenye kumbukumbu za Mazingira FM

Tuesday, 27 June 2023

Wakulima wa Pamba Kunzugu wamekubali yaishe!!!!

Wakulima wa zao la Pamba kata ya Kunzugu Halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara wamesema kutokana na ugumu wa maisha wameshindwa kuendelea kusubiri bei ya pamba ipande na badala yake wameamua kuuza kwa bei elekezi ya shilingi 1060

Wakizungumza na Radio Mazingira Fm jumapili hii 25 June 2023 katika ofisi za AMCOS Kunzugu 'Kituo B' wakati wakiuza pamba wakulima hao wamesema wamesubiri kwa muda mrefu kuona ushindani wa makampuni katika kupandisha bei lakini mpaka sasa hakuna kampuni iliyojitokeza kulipa zaidi ya bei elekezi ya shilingi 1060 iliyotangazwa na serikali.

Pambano Henga ni mkulima wa Pamba kata ya Kunzugu

"Kwa bei ya shilingi 1060 naona kwangu ni kama mzigo kwasababu ninapouza kilo 10 haikidhi mahitaji yangu kwahiyo pamba nimeshauza kulingana na shida niliyonayo hususani njaa" alisema Pambano Henga ambaye ni mkulima wa pamba.

Chaba Charles Chaba ni mkulima wa Pamba amesema "kulingana na matarajio yangu mwaka huu nilitarajia bei itakuwa kama mwaka jana lakini nimejikuta nanawia kalai, kwasababu mwaka jana tulikuwa na bei ya shilingi 2000 kwa kilo lakini mwaka huu imeshuka hadi kufikia shilingi 1060 kwa kilo kwahiyo nimeshindwa kufanya nilichotarajia baada ya kuuza pamba".

Wakulima wakiwa katika ofisi za AMCOS Kunzugu kwa ajili ya kuuza pamba

Mazingira Fm imezungumza na Katibu wa AMCOS katika kituo hicho, Nyang'era Lukiko amesema zoezi la ununuzi wa pamba wameanza tarehe 26 May 2023  ambapo wakulima walianza kwa kusuasua wakilalamikia bei iliyotangazwa lakini mpaka sasa wamenunua zaidi ya kilo 136,000 kutokana na ugumu wa maisha wengi wao wameshindwa kusubiri na kulazimika kuuza kwa bei iliyopo hivyo pamba katika eneo lao inakaribia kuisha.

Nyang'era amesema walitegemea kampuni 9 za ununuzi wa pamba wilaya ya Bunda zitashindana katika kupandisha bei ya pamba lakini mpaka sasa hazina ushindani badala yake kila kampuni inapanga foleni kwa AMCOS kwamba ikitoka kampuni fulani nyingine ikusanyiwe kwa bei hiyo hiyo ya shilingi 1060.


No comments:

Post a Comment

Chagua Unachotaka Kusoma

Mazingira FM Newsroom
HabariHabari za Bunda, Mara, Tanzania na jamii tunayohudumia. MichezoMatokeo, ligi, vipaji na habari za michezo. MazingiraUhifadhi, hali ya mazingira, kilimo na maendeleo. JamiiAfya, elimu, wanawake, vijana na maendeleo ya jamii.
Tufuate

Mazingira FM Mitandaoni

+255 621 046 491 • mazingirafm@gmail.com