Mahakama ya Wilaya ya Bunda imemuhukumu MASUBUGU MASUBUGU (32) MWIKIZU MKAZI WA BUNDA MJINI kifungo Cha miaka Thelathini jela na kuchapwa viboko 12 na kumlipa fidia muhanga ya shilingi milioni moja Kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 13
mwanafunzi wa darasa la Saba
Hukumu hiyo imetokewa Mnamo tarehe 30/05/2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda Mbele ya mheshimiwa Hakim mkazi Mfawidhi Mulokozi Kamuntu ambapo ni Kesi nambari 59/2023
Ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa serikali Toka jeshi la Police D/Sgt Athumani Salimu kuwa Mshtakiwa huyu alitenda kosa hilo tarehe 23/05/2023 majira ya saa 14:00hrs huko eneo la Mtaa wa Luselu ndani ya mji wa Bunda ambapo Mshtakiwa alimkamata mtoto huyo Kwa nguvu na kumuingiza kwenye Nyumba ya nyasi kisha kumbaka kwa nguvu.
Baada ya kumaliza tendo hilo la kinyama Mshtakiwa alitoka na kukimbia kusiko julikana.
Mtoto alitoa taarifa Kwa wazazi na kupelekwa Polisi kisha Hospitalin Kwa MATIBABU na uchunguzi.
Athumani alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo angalia akijua ni Kinyume na kifungu Cha 130 (1) (2) (e) na kifungu Cha 131 (1).
Mwendesha Mashtaka Athumani aliiomba Mahakama itoe adhabu kali Kwa Mshtakiwa Kwa kuwa matukio haya ya kinyama yamekuwa yakikithiri kwenye JAMII na KUHARIBU saikolojia ya watoto ambao ni viongizi wetu wa kesho ili owe fundisho Kwa Mshtakiwa na Kwa watu wengine wenye tabia kama yake.
Mshtakiwa Katika utetezi wake alikiri kitendo hicho na aliiomba mahakama kupunguziwa adhabu kwakuwa alipitiwa na kuwa Shetani ndiye aliyemlagai.
Baada ya maelezo hayo Mheshimiwa Mulokozi Kamuntu alisema mahakama imejilidhisha pasi na shaka kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo hivyo mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 30 kuchapwa 12 na kulipa fidia Kwa muhanga milioni moja
No comments:
Post a Comment