Mazingira Fm yawakosha watoto KKKT Bunda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 10 June 2023

Mazingira Fm yawakosha watoto KKKT Bunda

Watoto wa Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana KKKT Bunda wakiwa katika studio za Radio Mazingira Fm

 Watoto kutoka kituo cha Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana kanisa la KKKT Bunda leo 10 June 2023 wametembelea kituo cha Radio Mazingira Fm ili kujionea uendeshaji, maandalizi, urushaji wa vipindi pamoja na kushiriki katika kipindi cha Watoto.

Debora Patrick, Kiongozi wa Watoto Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijiana KKKT Bunda.

Wakizungumza baada ya kufika na kujionea shughuli mbalimbali katika kituo cha Radio Mazingira Fm, wamepongeza namna inavyoendesha shughuli zake na kuandaa vipindi vinavyogusa jamii.


"Tumejifunza vitu vingi sana hapa na nina furaha kubwa sana. Wito wangu kwa jamii tuendelee kuisikiliza Radio Mazingira kwasababu ni radio inayotoa taarifa za ukweli na ni radio ambayo ipo karibu na jamii yetu" Debora Patrick 

Makaranga Maduhu, Kiongozi wa Watoto Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijiana KKKT Bunda.


"Kituo hiki nimekipenda kwasababu kina matangazo mazuri na ninayo furaha kubwa mahali hapa nimejifunza vitu vingi kituo hiki kina matangazo mengi na mazuri na hauwezi kushindwa kuifatilia" Makaranga


No comments:

Post a Comment