Anusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday 9 June 2023

Anusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni.

 

Janeth Samweli (28) mkazi wa mtaa wa Kabarimu kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu na anayetajwa kuwa na mume wake tumboni kisha mwanaume huyo kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumza na Mazingira Fm mashuhuda wa tukio hilo wamesema ilikuwa ni majira ya saa tano za asubuhi leo june 8, 2023 eneo la Kabarimu mwanaume aliyetambulika kwa jina la Maiko alianza kuzozana na mke wake akimtuhumu kushirikiana na polisi ili akamatwe ndipo alipotoa kisu na kumchoma tumboni kisha kutokomea huku akiwa amewafungia wapangaji wenzake ndani wasiweze kutoa msaada

Mashuhuda

Naye baba mzazi wa Janeth amesema yeye anatambua kuwa mwanae anaishi na mwanaume lakini hajawai kumuona mwanaume huyo wala hajawai kufika kwake kujitambulisha kwamba yeye ndo anaishi na binti yake, hadi leo alipopata simu kwamba binti yake amejeruhiwa kwa kisu na mwanaume huyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kabarimu Ndugu Nyamsusa Nyamsusa amesema ni kweli tukio hilo limetokea ambapo Maiko Joseph amemchoma kisu cha tumboni mke wake Janeth Samweli na tayari majeruhi amepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu huku serikali ya mtaa ikiendelea kushirikiana na jeshi la polisi kumtafuta aliyetenda kosa hilo kwa kuwa alitoroka.

Nyamsusa Nyamsusa

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuacha kuchukua sheria mkononi na kama kuna tatizo ni vema kufika kwa viongozi kujua namna ya kumaliza migogoro ama tofauti zao.

No comments:

Post a Comment