Nyamakokoto yaweka marufuku kwa wenye nyumba kumpangisha mtu bila barua ya alikotoka. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 15 June 2023

Nyamakokoto yaweka marufuku kwa wenye nyumba kumpangisha mtu bila barua ya alikotoka.


Diwani wa kata ya Nyamakokoto Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe EMANUEL MALIBWA  amepiga  marufuku kwa wenye nyumba kuwapangisha watu bila  kuwa na uthibitisho wa barua alikotoka.

Akizungumza katika kikako cha  hadhara  mtaa wa barabara ya Ukerewe Halmashauri ya Mji wa Bunda katika mwendelezo wa ziara yake  amesema matukio ya wizi yaliyoshamili katika kata hiyo yanachangiwa na wenye nyumba kupangisha watu wasiyo waaminifu na wasiyofahamika walikotoka.

Amesema kuanzia sasa  mwenyenyumba yeyote atayepangisha mpangaji chumba bila taarifa watafikishwa polisi yeye na mpangaji wake.

Emmanuel Malibwa

Aidha Mhe Malibwa amesema uongozi wa kata itaanzisha oparasheni maalumu ya kusaka na kutawanya vijiwe vyote vya bangi ambavyo ndivyo vinavyochochea uharifu katika kata hiyo huku akiliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali wali wanaofikishwa kwao kwa makosa ya kujihusisha na masuala ya bangi.

Emmanuel Malibwa

Kwaupande wake D/Sgt  ATHUMAN SALIMU kwa niaba ya mkuu wa kituo cha polisi Bunda amewataka wananchi kushirikiana jeshi la polisi katika masuala ya ulinzi kwa kuwa jukumu la ulinzi ni lakila mtanzania kwa mujibu wa sheria

Hata hivyo amewataka wakazi wa Nyamakokoto kufuata utaratibu wakati wa kutoa taarifa za matukio la kihalifu ili kuweza kupata msaada wa haraka.

D/Sgt  ATHUMAN SALIMU

No comments:

Post a Comment