Wakulima wa pamba waishauri serikali itangaze bei ya kununua pamba kabla hawajalima. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday 2 June 2023

Wakulima wa pamba waishauri serikali itangaze bei ya kununua pamba kabla hawajalima.

 


Wakulima wa zao la pamba wilaya ya Bunda wameishauri serikali kutangaza bei ya pamba mwanzoni mwa msimu kabla ya kuanza kulima

Akizungumza na Mazingira Fm katika kituo cha AMCOS Balili mwalimu Tumaini Nyangamba Ndaro ambaye ni mkulima amesema ni vema serikali ikawa inatangaza bei ya kununua pamba mapema ikiwezekana mwanzoni kabla wakulima hawajaanza kulima pamba ili kutokana na bei hiyo mkulima aamue kulima au kuacha tofauti na ilivyo sasa

Tumaini Ndaro

Akizungumzia kuhusu bei ya mwaka huu tumaini amesema imekuwa chini sana ukilinganisha na bei ya mwaka jana lakini pia msimu huu umekubwa na changamoto ya kuchelewa kwa mvua

Kwa upande wake katibu wa AMCOS Balili Samweli Mari Chacha amesema tangu kufunguliwa kwa msimu tarehe 23 May wakulima wamekuwa wachache wanaopeleka pamba kwenye AMCOS kuuza ikilinganishwa na mwaka jana ambapo amesema kwa wastani wanapokea wakulima 10 hadi 16 kwa siku huku wakipima kilo 7000 kwa siku tofauti na mwaka jana ambapo walikuwa wakipima hadi kilo zaidi ya 1500 hadi 2000 kwa siku.

Samwel Mari Chacha

No comments:

Post a Comment