Diwani akabidhi mabomba ya maji yenye urefu wa mita 950 eneo a kisiwani kata ya Manyamanyama - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 7 June 2023

Diwani akabidhi mabomba ya maji yenye urefu wa mita 950 eneo a kisiwani kata ya Manyamanyama

 

Diwani wa kata ya Manyamanyama Mhe Mathayo Machilu amekabidhi mabomba ya maji yenye urefu wa mita 950 eneo la kisiwani Mtaa wa Mbugani kata ya Manyamanyama.

Akizungumza katika kikao hicho Cha kukabidhi mabomba hayo Mhe Machilu amesema kama alivyoahidi katika kipindi Cha kampeni za uchaguzi 2020 katika Mtaa wa Mbugani hasa eneo la kisiwani lilikuwa na Changamoto ya Maji, barabara na umeme

MATHAYO MACHILU

Aidha amewapongeza wakazi wa eneo la kisiwani kwa kujitolea kwa michango yao iliyowezesha kupatikana kwa mabomba hayo yenye urefu wa mita 950 yameghalimu shilingi (2,565,500) milioni mbili laki Tano na elfu sitini na Tano na mia tano.

MATHAYO MACHILU

Kwa upande wao wakazi wa kisiwani wamesema tatizo la ukosefu wa huduma za kijamii ni changamoto kubwa sana licha ya kuwa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Aidha wakazi hao wamesema tatizo kubwa ni ukosefu wa umeme, Maji pamoja na Barabara hivyo ujio wa mabomba ya maji yamewatia moyo sana.

WANANCHI WA KISIWANI

No comments:

Post a Comment