Wakazi wa Nyamakokokoto watakiwa kununua milango 15 iliyoibiwa shule za Balili na Bunda. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 21 June 2023

Wakazi wa Nyamakokokoto watakiwa kununua milango 15 iliyoibiwa shule za Balili na Bunda.

 

Emmanuel Malibwa

Diwani wa kata ya Nyamakokoto Emmanuel Malibwa amewataka wakazi wa kata hiyo kuchangia utengenezaji wa milango 15 ya vyoo iliyoibiwa katika shule za msingi za balili na bunda.

Akizungumza na radio mazingira fm katika kutamatatisha ziara yake ndani ya mitaa minne amesema tukio la wizi wa milango 15 ya vyoo katika shule za msingi za balili na bunda ni la ajabu na kwa kuwa wananchi waliona wizi huo unafanyika na hawakuchukua hatua ni vema wakainunua

Amesema serikali ilitoa fedha za ujenzi wa vyoo ambapo wananchi hawakuchangia chochote sasa kwa kuwa hawakuona uchungu na serikali haiwezi tena kutoa fedha kununua milango mingine nay eye kama diwani hayuko tayari kuona watoto wanapata shida, basi wazazi watawajibika kuitengeneza milango hiyo

Emmanuel Malibwa

Aidha Mhe Malibwa amesema katika ziara yake ndani ya mitaa minne inayounda kata ya Nyamakokoto changamoto kubwa aliyokutana nayo ni suala la usalama ambapo amebainisha kuwa wenye nyumba kupangisha wapangaji wasiokuwa waaminifu hivyo ametoa maelekezo kwa wenye nyumba wote kata ya Nyamakokoto ni marufuku kumpangisha mtu asiyekuwa na kibali kwa maana ya barua ya mwenyekiti anakotoka ikiwa na muhuri na namba za simu.

Emmanuel Malibwa

No comments:

Post a Comment