Neema ya barabara za lami Bunda ni kilometa 25 za mitaa - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Sunday 2 July 2023

Neema ya barabara za lami Bunda ni kilometa 25 za mitaa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dk Vicent Naano amesema serikali imeleta fedha kwa ajiri ya ujenzi wa barabara kilometa 25 za lami ndani ya barabara za mitaa Bunda mjini,  stendi mpya ya kisasa, soko, pamoja na machinjio.

Dc Naano ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara aliyoufanya kata ya Kabarimu alipofika kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao

Dk Vicent Naano

Aidha amewataka wafanyabiashara wa mbao, uchomeleaji, watengenezaji wa fenicha kujiandaa kwa kuwa watalazimika kuondoka mjini kati ili mji uweze kupangwa vizuri

Dk Vicent Naano

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliongozana na viongozi kutoka taasisi zote za umma ikiwa ni pamoja na BUWSSA, TASAF, TANROAD, KILIMO na MIFUGO miongoni mwa taasisi zingine.

Katika hatua nyingine DC Naano amewataka wataalamu kutoka halmashauri na taasisi za serikali kushughulikia changamoto za wananchi ili kuepusha migogoro.

No comments:

Post a Comment