Mmoja afariki 46 wajeruhiwa ajali ya gari Bunda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 5 July 2023

Mmoja afariki 46 wajeruhiwa ajali ya gari Bunda

 

Wahudumu wa hospitari ya Bunda DDH wakisaidia harakati za kuwaokoa majeruhi wa ajali, Picha na Adelinus Banenwa

Mtu mmoja Anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amepozea  maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari  walilokuwa  wakisafiria kupata ajali katika eneo la Balili kona Bunda mkoani Mara

Na Adelinus Banenwa

Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Johamvia linalofanya safari zake kutokea Kemgesi tarafa ya Ikorongo wilayani Serengeti kwenda Mwanza .

Ajali hiyo imetokea leo July 5, 2023 majira ya asubuhi katika eneo la Balili kona mjini Bunda baada ya dereva kudaiwa kushindwa kupiga kona.

majeruhi wamesema gari hilo licha ya kuwa na kwenda kasi aliyokuwa nao dereva bado gari hilo lilikuwa na changamoto nyingi

Mganga mkuu kutoka hospitali ya Bunda DDH Dkt Pendo Faustine amesema hospitali hiyo imepokea mwili wa kijana mmoja wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25  ambaye jina lake halijatambulika pia majeruhi 46 ambapo watano kati yao wamepewa rufaa kwenda Bugando kutokana na hali zao kuwa mbaya na 41 wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na hali zao zinaendelea vizuri

Gari lililopata ajali, Picha na Adelinus Banenwa
Mganga mkuu kutoka hospitali ya Bunda DDH Dkt Pendo Faustine
Wakazi wa balili waliofika eneo la ajali kutoa msaada, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa mujibu wa mashuda  wa ajali hiyo wameiambia mazingira fm kuwa gari hilo lilikuwa mwendo kasi hivyo baada ya kufika kwenye kona inawezekana bleki ziligoma hivyo kupelekea kumshinda dereva na kupinduka

Shabani Daudi Charles mkazi wa balili shuhuda wa ajali

Kwa upande wao baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakizungumza na mazingira fm  wamesema gari hilo licha ya kuwa na kwenda kasi aliyokuwa nao dereva bado gari hilo lilikuwa na changamoto nyingi kwa kuwa ilipofika mugeta ililazimika kusimama kutokana na gari hilo kutoka moshi mwingi.

sauti za baadhi ya majeruhi wa ajali

Radio Mazingira FM bado inaendelea na jitihada za kumtafurta kamanda wa polisi mkoa wa Mara kufafanua zaidi kuhusu chanzo cha ajali na athari za ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment