![]() |
![]() |
Pambano Henga ni mkulima wa Pamba kata ya Kunzugu |
![]() |
Wakulima wakiwa katika ofisi za AMCOS Kunzugu kwa ajili ya kuuza pamba |
![]() |
![]() |
Pambano Henga ni mkulima wa Pamba kata ya Kunzugu |
![]() |
Wakulima wakiwa katika ofisi za AMCOS Kunzugu kwa ajili ya kuuza pamba |
Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe Said Mtanda ametoa siku kumi na nne 14 kwa halmashauri ya mji wa Bunda na halmashauri ya wilaya Bunda kufanya mgawanyo wa mali na madeni ili kuondoa mkanganyiko uliopo kwa sasa.
Hayo ameyasema leo katika baraza maalumu la madiwani la halmashauri ya Mji wa Bunda lililokaa kujadiri taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa mkuu wa hesabu za serikali CAG hoja za mwaka 2021 na 2022 ambapo kwa halmashauri ya mji wa Bunda ilikuwa na hoja 35 ambapo kati ya hizo hoja 12 zimefungwa huku hoja 23 zikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Mhe Mtanda amesema anawaelekeza wakurugenzi wa halmashauri zote mbili Bunda mji na Bunda wilaya kukaa na kufanya mchanganuo wa mali na madeni huku akimtaka katibu tawala wa mkoa kusimamia zoezi hilo ndani ya siku 14 liwe limekamilika.
Aidha amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda kutengeneza gari mali ya halmashauri hiyo lililotelekezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja ili litumike kufanya kazi za halmashauri ambapo awali mpango wa halmashauri ilikuwa kuliuza.
Aidha ameipongeza halmashauri ya mji wa Bunda kwa kupata hati safi mfurulizo pia kwa kufikia asilimia 92 ya makusanyo huku akisema anaamini watavuka malengo katika makusanyo hayo.
Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Mara, Geofrey Comoro amewaasa wafanyabiashara wasisubiri siku ya mwisho kufanya malipo ya kodi ya mapato bali wafanye mapema ili kuepuka faini na usumbufu usio wa lazima.
Comoro ameyasema hayo leo tarehe 21 June 2023 kupitia mahojiano na Radio Mazingira Fm katika kipindi cha asubuhi leo akihamasisha Ulipaji wa kodi ya mapato awamu ya pili 2023 na Uwasilishaji wa Ritani 2022.
Wito umetolewa kwa vijana kumtanguliza Mungu katika shughuli zao na kujiepusha na mambo yasiyofaa katika jamii
Hayo yamesemwa mwenyekiti wa vijana kanisa la FPCT neno la Neema Bade Winford chini ya mchungaji Omoso Tukiko ikiwa ni hitimisho la wiki ya vijana iliyoanza tarehe 12 june na kutamatika 18 june 2023.
Bade amesema ujumbe mkubwa walikuwa nao wiki nzima ni mahusiano ya kijana pasipo kuathiri utaratibu wa Mungu na kanisa , uchumi wa kijana , pia kumtanguliza Mungu katika kila hatua.
Kwa upande wao vijana wamesema wamejifunza mambo mengi japo wanao muda mrefu katika kumtumikia Mungu lakini kupitia wiki ya vijana kuna jambo jipya wamejifunza
Aidha wamesema changamoto kubwa waliokutana nayo kwa vijana ni kutofanya kazi na badala yake kujiwekeza katika michezo ya kubahatisha, kamali, pamoja na ulevi.
Awali akisoma taarifa ya vijana Ester Gideon ambaye ni mkuu wa kitengo cha hamasa na habari idara ya vijana kanisani hapo amesema katika kipindi cha miezi sita idara ya vijana imefanya mambo mbalimbali ikiwepo kufanya uinjilisti , elimu kwa vijana na mazingira yake , kuhamasisha vijana kufanya kazi halali bila kuathiri uhusiano wao na Mungu.
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kimefanya mkutano katika kata ya bunda stoo halmashauri ya mji wa bunda huku wakigusia mambo mbalimbali likiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na ugumu wa maisha.
Katika mkutano huo ulioudhuriwa na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata hadi taifa akiwemo mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema Taifa John Pambalu, katibu mkuu wa Vijana Taifa Yohana kaunya miongoni mwa viongozi wengine
Akizungumza katika mkutano huo Yohana Kaunya ambaye alikuwa mgombea udiwani kata ya Bunda stoo katika uchaguzi mkuu 2020 na katibu mkuu CHADEMA Taifa amesema amekuja kuwashukuru wakazi wa kata ya Bunda stoo kwa kura walizompa pia amesema ukosefu wa ajira bado ni changamoto ili hali vijana wasomi wapo.
Aidha katibu huyo wa vijana amesema amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa kata ya Bunda stoo kuhusu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bili ya maji kuwa juu, ubovu wa miundombinu ya barabara, changamoto ya watu TASAF miongoni mwa changamoto zingine.
Naye mwenyekiti wa BAVICHA John Pambalu amesema kuwa tatizo la ugumu wa maisha bado ni kubwa sana katika taifa pia ukosefu wa ajira kwa vijana kunasababisha vijana wengi kushindwa kufanya kazi badala yake wanakwenda kwenye michezo ya kubahatisha
Aidha amesema baraza la vijana chadema litaadhimisha siku ya vijana duniani mkoani mbeya ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 12 August ambapo amewataka vijana kukutana ili kujua mustakabali wao.
Diwani wa kata ya Nyamakokoto Emmanuel Malibwa amewataka wakazi wa kata hiyo kuchangia utengenezaji wa milango 15 ya vyoo iliyoibiwa katika shule za msingi za balili na bunda.
Akizungumza na radio mazingira fm katika kutamatatisha ziara yake ndani ya mitaa minne amesema tukio la wizi wa milango 15 ya vyoo katika shule za msingi za balili na bunda ni la ajabu na kwa kuwa wananchi waliona wizi huo unafanyika na hawakuchukua hatua ni vema wakainunua
Amesema serikali ilitoa fedha za ujenzi wa vyoo ambapo wananchi hawakuchangia chochote sasa kwa kuwa hawakuona uchungu na serikali haiwezi tena kutoa fedha kununua milango mingine nay eye kama diwani hayuko tayari kuona watoto wanapata shida, basi wazazi watawajibika kuitengeneza milango hiyo
Aidha Mhe Malibwa amesema katika ziara yake ndani ya mitaa minne inayounda kata ya Nyamakokoto changamoto kubwa aliyokutana nayo ni suala la usalama ambapo amebainisha kuwa wenye nyumba kupangisha wapangaji wasiokuwa waaminifu hivyo ametoa maelekezo kwa wenye nyumba wote kata ya Nyamakokoto ni marufuku kumpangisha mtu asiyekuwa na kibali kwa maana ya barua ya mwenyekiti anakotoka ikiwa na muhuri na namba za simu.
Umoja wa vijana kanisa la FPCT Neno la neema chini ya mchungaji Omoso wametembele wodi ya wazazi kituo cha afya bunda ikiwa ni sehemu ya sherehe za wiki ya vijana kanisani hapo
Akizungumza na radio mazingira fm mwenyekiti wa vijana wa kanisa hilo Bade Winford amesema katika wiki hiyo ya vijana wamefanya mambo mengi ikiwemo kueneza habari njema za injili kwa vijana, michezo , pamoja na tukio la leo la kutembelea wodi ya wazazi kituo cha afya cha bunda ambapo wanatambua mchango wao wa kuendeleza uumbaji wa mungu.
Aidha amesema wiki hiyo ya vijana ilianza tangu tarehe 12 mwezi June na inatarajia kutamatika hapo kesho june 18 Kwa ibada itakayoongozwa na vijana.
Kwa upande wao akina mama waliojifungua kituo cha afya wameshukuru vijana wa FPCT Neno la Neema kuja kuwatembelea pia zawadi walizowaletea kwa maana ni mara chache sana kwa vijana kuwa na moyo kama huo pia wamewashukuru madaktari na wauguzi wanaowahudumia maana wanapata huduma nzuri pindi wanapofika kujifungua.
Diwani wa kata ya Nyamakokoto Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe EMANUEL MALIBWA amepiga marufuku kwa wenye nyumba kuwapangisha watu bila kuwa na uthibitisho wa barua alikotoka.
Akizungumza katika kikako cha hadhara mtaa wa barabara ya Ukerewe Halmashauri ya Mji wa Bunda katika mwendelezo wa ziara yake amesema matukio ya wizi yaliyoshamili katika kata hiyo yanachangiwa na wenye nyumba kupangisha watu wasiyo waaminifu na wasiyofahamika walikotoka.
Amesema kuanzia sasa mwenyenyumba yeyote atayepangisha mpangaji chumba bila taarifa watafikishwa polisi yeye na mpangaji wake.
Aidha Mhe Malibwa amesema uongozi wa kata itaanzisha oparasheni maalumu ya kusaka na kutawanya vijiwe vyote vya bangi ambavyo ndivyo vinavyochochea uharifu katika kata hiyo huku akiliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali wali wanaofikishwa kwao kwa makosa ya kujihusisha na masuala ya bangi.
Kwaupande wake D/Sgt ATHUMAN SALIMU kwa niaba ya mkuu wa kituo cha polisi Bunda amewataka wananchi kushirikiana jeshi la polisi katika masuala ya ulinzi kwa kuwa jukumu la ulinzi ni lakila mtanzania kwa mujibu wa sheria
Hata hivyo amewataka wakazi wa Nyamakokoto kufuata utaratibu wakati wa kutoa taarifa za matukio la kihalifu ili kuweza kupata msaada wa haraka.
Watoto wa Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana KKKT Bunda wakiwa katika studio za Radio Mazingira Fm |
![]() |
Debora Patrick, Kiongozi wa Watoto Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijiana KKKT Bunda. |
Wakizungumza baada ya kufika na kujionea shughuli mbalimbali katika kituo cha Radio Mazingira Fm, wamepongeza namna inavyoendesha shughuli zake na kuandaa vipindi vinavyogusa jamii.
"Tumejifunza vitu vingi sana hapa na nina furaha kubwa sana. Wito wangu kwa jamii tuendelee kuisikiliza Radio Mazingira kwasababu ni radio inayotoa taarifa za ukweli na ni radio ambayo ipo karibu na jamii yetu" Debora Patrick
Makaranga Maduhu, Kiongozi wa Watoto Huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijiana KKKT Bunda. |
Janeth Samweli (28) mkazi wa mtaa wa Kabarimu kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu na anayetajwa kuwa na mume wake tumboni kisha mwanaume huyo kutokomea kusikojulikana.
Wakizungumza na Mazingira Fm mashuhuda wa tukio hilo wamesema ilikuwa ni majira ya saa tano za asubuhi leo june 8, 2023 eneo la Kabarimu mwanaume aliyetambulika kwa jina la Maiko alianza kuzozana na mke wake akimtuhumu kushirikiana na polisi ili akamatwe ndipo alipotoa kisu na kumchoma tumboni kisha kutokomea huku akiwa amewafungia wapangaji wenzake ndani wasiweze kutoa msaada
Naye baba mzazi wa Janeth amesema yeye anatambua kuwa mwanae anaishi na mwanaume lakini hajawai kumuona mwanaume huyo wala hajawai kufika kwake kujitambulisha kwamba yeye ndo anaishi na binti yake, hadi leo alipopata simu kwamba binti yake amejeruhiwa kwa kisu na mwanaume huyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kabarimu Ndugu Nyamsusa Nyamsusa amesema ni kweli tukio hilo limetokea ambapo Maiko Joseph amemchoma kisu cha tumboni mke wake Janeth Samweli na tayari majeruhi amepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu huku serikali ya mtaa ikiendelea kushirikiana na jeshi la polisi kumtafuta aliyetenda kosa hilo kwa kuwa alitoroka.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuacha kuchukua sheria mkononi na kama kuna tatizo ni vema kufika kwa viongozi kujua namna ya kumaliza migogoro ama tofauti zao.
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe |
Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wakati akifanya mahojiano na Radio Mazingira Fm hii leo tarehe 8 june 2023 kupitia Kipindi Cha Safari Mseto katika hatua za maandalizi ya chama hicho kuelekea katika mkutano wake wa hadhara uwanja wa shule ya msingi Mkendo mjini Musoma.
Zitto amesema kwa msimu uliopita bei ya pamba ilifika shilingi elfu mbili (2000) lakini katika msimu huu bei elekezi ni shilingi 1060 hivyo imepelekea malalamiko ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.
"Jana tulipokuwa Busega mkoani Simiyu tulitoa mapendekezo na la rahaka ni kuhakikisha bodi ya pamba na wizara ya kilimo wafanyie kazi suala la tija kwasababu wakulima wetu wanazalisha pamba chache sana katika kila hekari moja inayolomwa" amesema Zitto.
Zitto amesema wameishauri bodi ya pamba na wizara ya kilimo kuangalia suala la kilimo cha tija kwa kupata mazao mengi katika hekari moja na kuongeza thamani ya pamba kwa kuuza bidhaa zitokanazo na pamba mfano vitambaa.
Aidha ameishauri serikali kuwa na fao la bei kwa wakulima (Price Stabilisation) pale ambapo bei inapokuwa imeporomoka kwenye soko la dunia kiasi cha mkulima kushindwa kurejesha gharama zake, mfuko wa hifadhi za jamii umlipe ile hasara.
Zitto Kabwe yuko mkoani Mara katika mwendelezo wa uzinduzi wa mikutano ya hadhara walioanza tangu lilipoondolewa katazo la mikutano hiyo ni huu ukiwa ni mkoa wa 16 tangu waanze ziara hiyo mwezi February 2023
Zitto Kabwe katika studio za Radio Mazingira FM |
Chama Cha ACT Wazalendo kesho tarehe 8 June 2023 kitafanya mkutano mkubwa wa siasa katika Viwanja vya shule ya msingi Mkendo Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.
Hii ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake tangu ilivyozindua mikutano hiyo mwezi February 2023 Jijini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa mikutano ya kisiasa.
Akizungumza na Radio Mazingira Fm kupitia kipindi Cha Asubuhi leo, Mratibu wa Mikutano na Afisa wa ACT – Wazalendo makao makuu, Ndugu Mussa Bakari ‘ Tembo’ amesema tangu kuondolewa zuio la mikutano ya hadhara chama kimefanya mikutano katika Mikoa 9 awamu ya kwanza na sasa katika awamu ya pili watafanya katika Mikoa 10.
Diwani wa kata ya Manyamanyama Mhe Mathayo Machilu amekabidhi mabomba ya maji yenye urefu wa mita 950 eneo la kisiwani Mtaa wa Mbugani kata ya Manyamanyama.
Akizungumza katika kikao hicho Cha kukabidhi mabomba hayo Mhe Machilu amesema kama alivyoahidi katika kipindi Cha kampeni za uchaguzi 2020 katika Mtaa wa Mbugani hasa eneo la kisiwani lilikuwa na Changamoto ya Maji, barabara na umeme
Aidha amewapongeza wakazi wa eneo la kisiwani kwa kujitolea kwa michango yao iliyowezesha kupatikana kwa mabomba hayo yenye urefu wa mita 950 yameghalimu shilingi (2,565,500) milioni mbili laki Tano na elfu sitini na Tano na mia tano.
Kwa upande wao wakazi wa kisiwani wamesema tatizo la ukosefu wa huduma za kijamii ni changamoto kubwa sana licha ya kuwa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Aidha wakazi hao wamesema tatizo kubwa ni ukosefu wa umeme, Maji pamoja na Barabara hivyo ujio wa mabomba ya maji yamewatia moyo sana.
Namjungu Aloyce, mke wa Kalebu Dinda 'Otike' bodaboda aliyeuawa katika kijiji cha Nyakiswa kata ya Kyanyari Wilaya ya Butiama akisimulia hali ilivyokuwa |
Namjungu Aloyce ni mwanamke aliyepoteza mumewe katika tukio la mauaji ya watu wanne lililotokea tarehe 27 May 2023 Usiku katika kijiji Cha Nyakiswa kata ya Kyanyari Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Ndoto ya maisha marefu na mumewe iliishia usiku huo wa tarehe 27 wakiwa wameishi kwa takribani miaka 11 na kifanikiwa kupata watoto jumla ya watoto 5 wa kiume wanne na wakike mmoja wa kwanza akiwa na miaka sita.
Ni kwa kazi hiyo hiyo ya bodaboda ndio ilikuwa tegemeo la familia lakini katika usiku wa siku hiyo ndoto za familia zinapotea baada ya kupigiwa simu kuwa walichoweza kukiona ni ndala peke yake zikiwa zimetelekezwa kando ya barabara kabla ya masaa machache kutaarifiwa kuwa "Kalebu Dinda" amepatikana akiwa ameuawa.
"Nikiwa nimelala kama saa tano hivi alikuja mke wa shemeji yangu akanigongea mlango nilipofungua akaniuliza mumeo yuko wapi..nikamjibu sijui alipoondoka hapa ameniacha nimebandika 'fugo' (sufuria ya kupikia ugali) hadi sasa hivi sijamuona"
"Nilianza kumpigia simu ikawa inaita lakini hapokei nikahisi huenda yuko kwenye pikipiki hawezi kupokea kama ilivyo kawaida yake anapokuwa anaendesha...hadi baadaye alipotaarifiwa kuwa amepatikana akiwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mahindi"
Hii imeibua msiba mkubwa katika familia kwa baba ambaye hakupata hata sekunde ya kusema neno la mwisho kwa familia yake isipokuwa yale waliozungumza naye jioni kabla ya kuuawa.
Namjungu anasema mumewe alikwenda nyumbani kuwajulia hali ambapo mwanaye mkubwa alimweleza kuwa anaumwa ndipo 'Otike' akatoa maelekezo kwa mama yao ili kumnunulia dawa kutoka kwenye chenji iliyokuwa imebaki lakini alijibiwa kuwa imetumika kwenye mambo mengine.
Akiwa anatafakari namna ya kupata dawa kwa wakati kutokana na uhaba wa maduka ya dawa katika maeneo hayo aliondoka katika ishara ya kuendelea na kazi ya kutafuta mkate wa kila siku huku akiacha neno la matumaini kwa familia yake kuwa anapambania mahitaji yao.
"Akasema huko ninakokwenda hamna dawa laakini mtoto akamkandamizia kuwa baba kaninunulie dawa...alivyomwambia hivyo akaondoka akapandisha juu..." anasimulia Namjungu
Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kuongea na familia yake na kama Mungu angewafunulia kile ambacho kitafuata baada ya hapo huende wangemwambia maneno mazito yale yanayochemsha mioyo yao kwa sasa.
Akizungumza na Mazingira Fm anasema majira ya saa 5 usiku aligongewa mlango na ndugu zake wakimuuliza iwapo ana taarifa zozote kuhusu mumewe ndipo walipomwambia kuna taarifa za bodaboda kuvamiwa barabarani lakini mpaka wakati huo walikuwa wamefanikiwa kupata pikipiki ikiwa imetelekezwa barabarani na ndala nyeusi ambazo alithibitisha kuwa ni za mumewe.
Katika tukio hili vyombo vya dola vinaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaka waliohusika na mauaji hayo lakini kwa upande wa Namjungu anafikiria zaidi kuhusu hatima ya watoto wake ikiwa hakuwa na shughuli yoyote mbali na kilimo kwa ajili ya kujikimu kwa chakula.
Hivyo anatamani kuona sambamba na juhudi za kuimarisha ulinzi zinazofanywa na vyombo vya dola anatamani pia kuona ni kwa namna gani suala la malezi ya watoto linaangaliwa.
"Ninaomba mnisaidie kuwatafuta yaani hata kama ni kunyongwa na wenyewe kwasababu na wenyewe wameniumiza sana....ameniachia watoto wadogo..." anasimulia Namjungu kisha anahitimisha kwa kilio cha uchungu.
Katika tukio hilo watu watatu waliouawa akiwemo mume wa Namjungu (Kalebu Dinda au Otike) walikuwa ni waendesha bodaboda ambao tayari mazishi yao yamefanyika na pikipiki zao zilipatikana katika maeneo ya tukio huku mtu wa nne akiwa bado hajatambulika na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Butiama.
Wakulima wa zao la pamba wilaya ya Bunda wameishauri serikali kutangaza bei ya pamba mwanzoni mwa msimu kabla ya kuanza kulima
Akizungumza na Mazingira Fm katika kituo cha AMCOS Balili mwalimu Tumaini Nyangamba Ndaro ambaye ni mkulima amesema ni vema serikali ikawa inatangaza bei ya kununua pamba mapema ikiwezekana mwanzoni kabla wakulima hawajaanza kulima pamba ili kutokana na bei hiyo mkulima aamue kulima au kuacha tofauti na ilivyo sasa
Akizungumzia kuhusu bei ya mwaka huu tumaini amesema imekuwa chini sana ukilinganisha na bei ya mwaka jana lakini pia msimu huu umekubwa na changamoto ya kuchelewa kwa mvua
Kwa upande wake katibu wa AMCOS Balili Samweli Mari Chacha amesema tangu kufunguliwa kwa msimu tarehe 23 May wakulima wamekuwa wachache wanaopeleka pamba kwenye AMCOS kuuza ikilinganishwa na mwaka jana ambapo amesema kwa wastani wanapokea wakulima 10 hadi 16 kwa siku huku wakipima kilo 7000 kwa siku tofauti na mwaka jana ambapo walikuwa wakipima hadi kilo zaidi ya 1500 hadi 2000 kwa siku.