Wananchi Bunda stoo walidhishwa na huduma ya umeme ya REA - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 9 January 2018

Wananchi Bunda stoo walidhishwa na huduma ya umeme ya REAWananchi wa kata Bunda stoo katika halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa Mara wameeleza namna wamenufaika na huduma ya umeme wa REA ikiwa ni pamoja na kijipatia maendeleo ya kiuchumi kutokana na huduma hiyo.
Hayo yamesemwana baadhi ya wananchi wa mashine ya maji na migungani wakati wakizungumza na mazingira hii leo wamesema huduma ya umeme wa REA umewafikia walengwa kwa gharama nafuu ya elfu ishirini na saba kuvuta umeme huo ambapo huduma hiyo imeanza mwaka jana .

Wameongeza kuwa wengi wao katika maeneo hayo wamenufaika na uhuduma hiyo na wanafaaidika kutokana na huduma hiyo kuwasaidia katika matumizi ya nyumbani ikiwemo mwanga na kuchaji simu pia wanajipatia uchumi kupitia huduma hiyo ikwa ni pamoja na miradi inayotegemea umeme huo kama kuchajisha simu kuwaingizia kipato.

Aidha wamemuomba diwani wa kata ya bunda stoo kutembelea wakazi wa maeneo hayo kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo tatizo la maji ambapo limekuwa tatizo katika maeneo mbalimbali ya mji wabunda.

No comments:

Post a Comment