Msako wa jeshi la polisi wakimbiza Wakazi Wilayani Bunda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 16 January 2018

Msako wa jeshi la polisi wakimbiza Wakazi Wilayani BundaWAKAZI wengi wa Kijiji cha Mekomariro, katika wilaya ya Bunda mkoani Mara, hususani wanaume wameyakimbia makazi yao na kutokana na msako wa Jeshi la Polisi wa watuhumiwa wa mauaji.

Msako huo unaendeshwa kufuatia mauaji ya watu wawili wakazi wa wilyani Serengeti, wanaodaiwa kuuawa na watuhumiwa wanaodaiwa kuwa ni wakazi wa kijiji hicho, ambapo chanzo kinadaiwa ni wizi wa mifugo iliyokuwa katika shamba lenye mgogoro wa ardhi kati ya wilaya ya Bunda, Serengeti na Butiama.

Hayo yalibainishwa juzi baada ya uongozi wa mkoa wa Mara kufika katika kijiji hicho, na kuelezwa kuwa wananchi wengi walikimbia msako wa Polisi, wakiwamo viongozi.

Waliotajwa kukimbia kamatakamata hiyo ni diwani wa kata hiyo, mwenyekiti wa kijiji na ofisa mtendaji wa kijiji hicho.

Kufuatia operesheni hiyo iiliyoanza Januari 12 majira ya jioni hadi usiku, baadhi ya wanakijiji walilalamikia polisi kwamba walitumia nguvu kubwa ikiwamo kuvunja nyumba zao, kuharibiwa mali na kuporwa baadhi ya mali zao zikiwamo fedha.


Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa kikiongozwa na mwenyekiti, Justine Rukaka; Katibu, Mabutu Malima na Mbunge wa Bunda Vijijini,  Boniphace Mwita Getere, walifika eneo la tukio na kulaani mauaji na kusikitishwa na nguvu kubwa waliyotumia polisi.

No comments:

Post a Comment