Mwanakwaya
wa kwaya ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Secilia, Kigango cha Muze
Parokia ya Zimba Jimbo la Sumbawanga, Flora Nandi (25), ameanguka na
kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa
kanisani.
Tukio hilo la kifo cha mwanakwaya huyo wa kwaya ya Mtakatifu Secilia lilitokea Jumapili saa 4 asubuhi wakati wa idada ya kwanza.
Akisimulia
tukio hilo Katekista wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Philipo
Lupadasi, alisema kuwa wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu muda mfupi
baada ya Lupadasi kutoka kutoa sadaka ya shukrani na kuendelea kuimba.
Alisema
ghafla aliangua chini hali iliyozua mtafaruku na kusababisha ibada
kusimama kwa muda mfupi, hali iliyowafanya wanakwaya wenzake kumnyanyua
na kumtoa nje ya kanisa, ili pate hewa wakiamini kuwa amepoteza fahamu.
Katekista
huyo alisema baada ya kumpepea kwa muda wanakwaya wenzake waliona Flora
hapati fahamu, hali iliyowalazimu kumkimbiza katika zahanati ya kijiji
cha Muze kwa ajili ya matibabu.
Alisema
baada ya kufikishwa katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya
na baada ya kufanyiwa uchunguzi ilibainika kuwa walimpeleka katika
zahanati akiwa ameshafariki dunia.
Baada
ya kupewa taarifa ya kifo hicho wanakwaya hao waliangua vilio hali
iliyosababisha washindwe kurudi kanisani kuimba katika ibada ya pili,
hivyo kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani kwake.
Katekista huyo alifafanua kuwa Flora wakati anafariki dunia alikuwa na ujauzito wa miezi mitano.
Kwa
upande wake mwalimu wa kwaya ya Mtakatifu Cecilia, Aloyce Mwandanje,
alisema kuwa kifo cha mwanakwaya mwenzao kimewaachia majonzi makubwa,
ingawa ni mapenzi ya Mungu.
Alisema mwili wa marehemu ulizikwa Jumatatu katika makaburi ya Kijiji cha Muze.
No comments:
Post a Comment