Zikiwa zimebaki siku tatu kuwasili kwa waziri mkuu
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu wilayani Bunda
mkoani Mara kwa ziara ya siku mbili wilayani hapa, mwananchi mmoja aliyejulikana kwa majina Bonphace
Chacha amekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusishwa na vitendo vya
rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama cha mapinduzi CCM mwenyekiti wa chama hicho Justine Rukaka
ameeleza kwamba wameita jeshi la polisi pamoja
na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru wilayani hapa na
kuwakabidhi mtuhumiwa huyo kutokana na
madai ya mazingira ya kuwepo viashiria vya vitendo vya rushwa baina yake na mkuu wa wilaya ya Bunda mwl Lydia
Bupilipili.
Mtuhumiwa huyo awali aliwekwa chini ya ulinzi na
wajumbe wa kamati ya siasa ya chama hicho kilichoketi leo baada ya mtuhumiwa
huyo kuonana na mwenyekiti wa CCM na kumweleza kwamba ametumwa na mkuu wa
wilaya kuwa aongee na viongozi wa kamati hiyo ili wasimjadili na anaomba msamaha kwa makosa
aliyoyafanya.
Redio Mazingira fm ilipotafutwa mkuu wa wilaya ya Bunda kuthibitisha taarifa hizo amesema kuwa hajui chochote
kuhusu madai hayo na hajamtuma mtu yeyote kumuombea msamaha ndani ya chama
hicho.
Hata hivyo ametoa onyo kwa wananchi kutokutumia jina lake
vibaya kwani yeye anashughulikia matatizo ya wananchi hivyo wananchi waungane
naye kuyatatua kwakuwa Bunda kuna matatizo mengi yanayotakiwa kushughulikiwa.
No comments:
Post a Comment