Waziri mkuu aapa kula sahani moja na mamlaka ya maji Bunda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 20 January 2018

Waziri mkuu aapa kula sahani moja na mamlaka ya maji BundaWaziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameapa kula sahani na Mamla ya Maji Bunda BUWASA.

Hii inajiri baada ya kutembelea moja ya eneo la mradi wa maji na kujionea udanganyifu uliofanyika huku akiambiwa kuwa mradi umefikia asimilika 98 suala ambalo waziri mkuu amesema si kweli.

Majira ya saa kumi na moja jioni Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amefanya Mkutano wa hadhara mjini Bunda katika Uwanja wa Sabasaba na kuwaeleza wananchi Kwamba serikali ilitoa shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya mradi wa maji lakini umeshindwa kukamilika licha ya kuwa mradi huo ni wa muda mrefu.

Waziri mkuu amesema serikali haina nafasi ya kuwavumilia wale wote wanaoharibu miradi ambayo serikali imetoa pesa ili kuwasaidia wananchi wake hivyo kabla wananchi hawajapata madhara mtu huyo au watu hao wataondolewa mara moja kwani inaonekana wazi wameshindwa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuwatumikia wananchi.

Kutokana na kutokuridhishwa na mradi wa maji Bunda Waziri Mkuu  ameagiza Mkandarasi wa mradi huo,meneja wa maji Bunda ,Mhasibu wa Buwasa},Meneja wa majiMusoma ,Mhasibu MUWASA}, Wabunge wa majimbo yote matatu ya wilaya ya Bunda pamoja na Mkuu wa wilaya Mwl, Lydia Bupilipili wakutane ikulu kujadili suala hilo la maji kwa kina kabla hajachukua mamuzi.

Pamoja na hayo Waziri mkuu amewakumbusha vijana wa kiume kuwa miaka 30 iko palepale kwa yeyote ambaye atampa mimba mwanafunzi.
  No comments:

Post a Comment