Waziri wa
Tanzania Mh Kassim Majaliwa ametoa Siku 08 kwa Kamishena wa TRA kuhakikisha
anamfikisha mkandarasi aliyehuska kujenga jengo la TRA Sirari ambapo ni mpakani
mwa Tanzania na Kenya baada ya kutembelea eneo hilo na kutolidhishwa na ujenzi
wake huku akienda na taarifa zote jinsi alivyokuwa akilipwa fedha hizo.
Hayo
yamebainishwa leo mara baada ya Waziri kuweka jiwe la msingi katika kituo cha
Afya Sirari na kutembelea jingo hilo na kutoa kauli hiyo kuhusu ujezni wa jingo
hilo la TRA Sirari mpakani mwa Nchi ya Kenya na Tanzania.
Awali waziri
huyo ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha Afya Sirari baada
ya Serikali kupeleka Millioni Miatano Mfuko wa Jimbo la Tarime vijiji
kupitia mbunge wake John Heche ukatoa Millioni Mianne na Wananchi kuchangia
Millioni Mianne Waziri huyo naye aklachangia Millioni Miatano ili kuongeza
Ngunvu na kusema kuwa Serikali nayo inatoa Shilingi millioni Miambili Themanini
kwa ajili ya ununuzi waVifaa huku akipongeza ujenzi wa kituo hicho cha Afya.
Pia Waziri
amesema kuwa serikali itawachukulia hatua kali wale wanaendelea kukatisha ndoto
za watoto wa kike hapa Nchini.
Aidha Mbunge wa
Jimbo la Tarime Vijiji CHADEMA John Heche akaomba Waziri kuruhusu uuzaji wa
nafaka yakiwemo mahindi Nchi jirani ya Kenya huku Mbunge wa Jimbo la Tarime
Mjini Esther Matiko CHADEMA akiwapongeza wananchi wa Sirari kwa kujitoa katika
ujenzi wa Kituo cha Afya na kuomba Serikali kuendelea kuwaunga Mkono wanachi
katika ujenzi wa Miundombinu ya Afya naElimu.
Waziri Mkuu bado
anaendelea na ziara yake Mkoani Mara ambapo kwa sasa bado yuko Wilayani Tarime
na ataelekea Serengeti baada ya kuongea na wakazi wa Nyamongo Kesho.
No comments:
Post a Comment