Mkuu wa Mkoa wa Mara azungumzia matukio ya ukatili yanayoendelea kutokea Ndani ya Mkoa Wake. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 9 January 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mara azungumzia matukio ya ukatili yanayoendelea kutokea Ndani ya Mkoa Wake.Wito umetolewa kwa Jamii  ya Mkoa wa Mara kutakiwa kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa serikali ili kuhakikisha kuwa vitendo wa ukatili wa kijinsia vinakomeshwa ndani ya mkoa huo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati akizungumza katika uzinduzi wa saccos ya wanawake wa halmashauri ya mji wa Bunda siku ya leo katika viwanja vya ofisi ya halmashauri hiyo.

Malima amesema hivi karibuni ndani ya mkoa wa Mara kumetokea matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike jambo ambalo sio la kuvumilikaa hata mara moja.

Aidha Malima amewasihi wa wanawake kuendelea na umoja walionao sasa ili wawe mfano hata kwa mikoa mingine katika kuelekea uchumi wa kati ndani ya nchi yetu.

Katika suala la uzinduzi wa SACCOS hiyo ofisi ya mkuu wa Mkoa imechangia Laki tano za kitanzania ili kuwawezesha wanawake hao katika kujikwamua kiuchumi.

Grace Marwa ambaye ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara yeye katika nafasi yake amekabidhi hati ya kiwanja chenye thamani ya Milioni Nne huku akiahidi kama saccos hiyo itaendelea vizuri atatoa mshahara wake wa miezi miwili kuwawezesha wanawake hao kukuza saccos yao.

Naye Mkurungezi wa mji wa Bunda Janeth mayanja amewahakikishia wanawake hao kuwa halmashauri ya mji wa bunda itafanya kazi kwa ukaribuni na Saccos hiyo ambayo ina jumla ya wanachama 450 na kwamba halmashauri imechangia milioni kumi katika saccos hiyo.

No comments:

Post a Comment