Serikali yaahidi kula sahani moja na watumishi wezi Mkoani Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 16 January 2018

Serikali yaahidi kula sahani moja na watumishi wezi Mkoani Mara



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.

 Amesema Serikali haikotayari kuwavumilia watumishi wanaojihusisha na wizi, ubadhilifu, rushwa na uzembe, hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

 Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Musoma mkoani Mara akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani hapa.

 Waziri Mkuu amewasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa mujibu wa sharia kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe vinachangia kupunguza kasi ya kuwaletea maendelea Watanzania.

 Amesema lengo ni kuhakikisha adhima ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi hususan wale wa hali ya chini inatimia, hivyo amewaagiza viongozi wa halmashauri wakiwemo Madiwani kusimamia vizuri miradi ya maendeleo.

 Pia Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara na watendaji wengine wa halmashauri kuacha tabia ya kukaa ofisini na dabala yake waende vijijini kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

 Waziri Mkuu amesema watendaji hao wanatakiwa waachane na tabia ya kuwasubiri wananchi wawapelekee malalamiko yao kwa sababu baadhi yao hawana uwezo wa kufika katika ofisi zao.

No comments:

Post a Comment