Saturday, 23 December 2017

Barabara bado ni changamoto katika kijiji cha Ruamkoma Wilayani Butiama


Wananchi wa kijiji cha  Ruamkoma kata ya Butiama Wilaya ya Butiama  mkoani  Mara wameiomba serikali kuwaboreshea miundombinu ya barabara katika kijiji hicho kwani wamekuwa wakishidwa kufanya shughuli za kimaendeleo katika kijiji hicho.

Hayo yamesemwa na wananchi wa kijiji wa ruamkoma wakati wakizungumza na mazingira fm kwa nyakati tofauti.

Mwikwabe Marwa ambae ni miongoni mwa wananchi hoa amesema kuwa wamekuwa wakipata shida kubwa ya kusafirisha bidhaa zao za biashara kutokana na ubovu wa barabara zilizopo katika kata hiyo na kuwalazimu kutumia gharama kubwa wakati wanapokuwa wanasafirisha bidhaa zao.


Aidha wamesema changamoto zingine wanazokumbana nazo ni pamoja na maji, umeme, na upungufu wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi na kuomba serikali kuwapelekea huduma hizo.

Mabwana Afya wanahitajika katika kijiji cha Sarama A wilaya ya Bunda

Wakazi wa kitongoji cha Mumwaro kijiji cha Sarama A wilaya ya Bunda Mkoani  Mara wameiomba serikali kuwapelekea mabwana afya katika kitongoji hicho ili waweze kuondokana na uchafunzi wa mazingira kwa kujisaidia ovyo aja kubwa na ndogo katika vichaka.

Kauli hiyo imetolewa na wananchi wa kitongoji hicho walipokuwa wakizungumza na mazingira fm.

Wambura kigunya ambaye ni miongoni mwa wakazi wa kitongoji hicho amesema kuwa wakazi wa kitongoji hicho walio wengi hawana vyoo kitendo kinacho wapelekea kujisaidia vichakani bila kujua ni hatari kwa afya ya zao.

Amesema kuwa ni vizuri kama serikali ya kitongoji ita kuwa na utaratibu wa kupita kila mji na kukagua kama kunachoo ili kuweza kunusuru afya za wakazi wa kitongoji hicho pia kuepuka magojwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na kuhara.

Hata hivyo  wameomba uongozi wa kitongoji hicho kuwachukulia hatua  za kisheria wale wote watakao bainika hawana choo katika miji yao ili iwe fundisho kwa wengine.


Thursday, 21 December 2017

Hizi ni salamu tosha kwa wahalifu wilayani Bunda katika musimu huu wa sikukuu

Jeshi la polisi wilayani Bunda Mkoani Mara limewahakikishia wananchi kuwa watasherekea sikukuu kwa amani na utulivu kwani wamejipanga kikamilrifu kukabiliana na wahalifu watakao taka kuchafua hali ya hewa katika musimu huu wa sikukuu.
Akizungumza kupitia kipindi cha Asubuhi leo kinachorushwa na kituo hiki Mkuu wa polisi Bunda kamanda Jeremiah Shila amesema wao kazi yao ni kuhakikisha wanalinda raia na mali zake hivyo katika musimu huu wa sikukuu wako makini sana katika suala la ulinzi kaika maeneo yote ya Wilaya ya Bunda lengo ni wananchi kuwa salama wakati wote.
OCD Shila amewatumia salama waharifu wote wanaopanga kuja kufanya uhalifu katika wilaya ya Bunda kuwa hata wasipoteze muda maana wao wamejiandaa kikamilifu.

OCD Shila pia amezungumzia suala la ulinzi na usalama Wilaya ya Bunda kufuati matukio mbalimbali kutokea hivi karibuni ikiwemo ya ukatili wa kijinsia yaliyojitokeza katika maeneo tofauti ndani ya wilaya ya Bunda na kusema kuwa wanayafanyia kazi matukio yote yaliojitokeza na kuomba wananchi kutochoka pindi polisi wanapotaka ushirikiano kutoka kwao.

Zao la Pamba Wilayani Bunda la wekewa mpango kazi wa kueleweka

Zao la pamba limesisitizwa sana na serikali kuhakikisha katika mikoa inayolima zao hilo linaongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa.

Katika Wilaya ya Bunda Mkoani Mara kupitia Mkuu wake wa Wilaya mwl. Lydia Bupilipili aliagiza kila mwananchi alime hekar mbili huku akiagiza shule zote msingi na sekondari kuwa na shamba la pamba, mbali na hivyo aliagiza Halmashauri zote Wilaya na Mji ziwe na shamba darasa .

Katika kutaka kujuwa zaidi hatua zilizofikiwa kupitia agizo la Mkuu wa Wilaya tumemtafuta Mkaguzi na Mratibu wa zao la Pamba wilaya ya bunda bwana liberatus soka amesema kuwa

Hatua iliyofikiwa ni nzuri kwa sababu asilimia kubwa walegwa wametekeleza agizo la Mkuu wetu wa wilaya kwahiyo tunatarajia mambo mazuri katika musimu huu wa kilimo hasa kilimo cha zao la Pamba’alisema Soka

Suala la Pembejeo feki wilayani Bunda kupatiwa majawabu.

Taasisi za serikali pamoja na taasisi Binafsi katika Wilaya ya Bunda Mkoani Mara wametakiwa kusimamia ipasavyo suala la pembejeo zinazotakiwa kuwafikia wa wakulima ili kuwawezesha kulima kilimo bora na sio bora kilimo.

Agizo hilo limetolewa Jana na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwalimu Lydia Bupilipili wakati akifungua wa mdahalo kuhusu Pembejeo feki Wilayani Bunda ulioandaliwa na Baraza la kilimo na mifugo Tanzania |Agricultural Council of Tanzania ] katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Bupilipili amesema Taasisi zinazohusika na usimamizi wa pembejeo wasipokuwa makini siku zote wataendelea kutiwa doa na wale wasiowatakia meme katika kazi yao hivyo amewataka kuamka nakuona sasa si muda wakufumbia macho masuala kama hayo.

Bupilipili amesema Wilaya ya Bunda inaongoza kwa pembejeo feki hivyo kuna kila sababu ya kuwa makini na watu wasio takia mema taifa lao kupitia kusambaza pembejeo feki kwa wakulima.


Bwana Khalid Ngassa kutoka Baraza La kilimo na mifugo Tanzania kwa upande wake amesema kuwa wakulima wanapata hasara kubwa na wanaumia sana kupitia pembejeo feki wanazopokea kutoka kwa wasambazaji hali ambayop inapelekea wakulima kukata tamaa na kilimo hivyo ameshauri wakulima nao wawe makini na pembejeo hizo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mapema kama wakigundua kunadosari popote.

Kwa upande wao wakulima wa Wilaya Bunda wamekubalia kwa kauli moja ya kufuata ushauri waliopewa ikiwa ni pamoja na kusema pale ambapo kuna kasoro ili wawahi kusaidiwa tatizo hilo.

Wednesday, 20 December 2017

vitendo vya ubakaji katika Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoni Mara bado vinaendelea kushika kasi

vitendo vya ubakaji katika Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoni Mara bado vinaendelea kushika kasi baada ya baba mmoja mwenye umri wa miaka 37 kuripotiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili katika kata ya nyamakokoto.
Akizungumza mtoto huyo jina tunalihifadhi amesema kuwa alikuwa akishawishiwa na baba huyo kwa kumpa hela, huku akikataa na hatimae siku moja akenda kuoga bafuni akamfanyia tendo hilo la ubakaji na kumweleza kuwa asitoe taarifa kwa wazazi wake kwani akifanya hivyo atamnyonga.
Aidha mama wa mtoto ameeleza kwamba alimuona mwanae akitembea akiwa ameachanisha miguu na kumuuliza ambapo mtoto huyo alimkimbia mama yake, hivyo alilazimika kumshawishi na kumweleza kwamba alibakwa na baba huyo.
Aidha baada ya kutoa taarifa polisi aliambiwa ampeleke mtoto hospitali kwa vipimo na kuonyesha kuwa ni kweli mtoto huyo amefanyiwa kitendo hicho.

Taarifa zilizopo ni kwamba alikamatwa na polisi mtuhumiwa huyo.

Tuesday, 19 December 2017

Mama amemficha mwanae ndani kwa sababu eti mwanae ni mgonjwa wilayani Bunda

Mama mmoja majina tunayahifadhi anaeishi katika Kata ya Nyamakokoto halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara ameripotiwa kumfanyia mwanae wa kumzaa kitendo cha unyanyasaji wa kijinsi kwa kumficha ndani huku akiwa mgonjwa hali iliyompelekea mtoto huo jina tumeliifadhi kudhoofika.
Mtoto huyo mwenye miaka 9,inaelezwa kuwa ana kg.16 tu.

Aidha afisa ustawi wa jamii halmashauri ya mji wa bunda Pius Masalu amekiri kupata taarifa za mtoto huyo na kuongeza kuwa baada ya kufuatilia ilibainika kuwa jina aliloandikishwa kupata dawa hospitalini hapo ilibadilishwa mfano alikuwa anaitwa musa baadae mama yake aliamua kubadilisha jina lake na kumwita adam.

Mwanafunzi amejikuta akiingia katika ulimwengu mpya baada ya kubakwa na Baba mdogo wake ambaye ndiye mlezi wilayani Bunda

Sasu  (si jina lake halisi) ni mwanafunzi wa Darasa la sita katika shule moja ya msingi iliyoko Wilayani Bunda mkoani Mara.
Mwanafunzi huyo alijikuta akiingia katika ulimwengu mpya baada ya kubakwa na Baba mdogo wake ambaye ndiye mlezi wa mtoto huyo tarehe 12 ya mwezi wa 12 mwaka 2016  wakati akiwa darasa la tano.
Baba mdogo alimchukua ili amlee wakati akiwa bado ni mdogo.
Kulingana na mwanafunzi huyo, Baba yake mdogo huyo mwenye wake wawili alianza kumfanyia kitendo hicho chA kinyama akiwa darasa la tano.
Kulingana na mwanafunzi huyo, mara kwa mara Baba mdogo huyo ambaye kwa wakati huo alikwa amemzidi umri kwa miaka kama 48, alimwimuita katika nyumba yake pindi walipo baki wawili nyumbani na kumlazimisha kufanya tendo hilo huku akimtishia kumuua endapo atasema kwa watu.
Baba huyo alizoea kumfanyia kitendo hicho hali ambayo iliendea kumuumiza mwanafunzi huyo na ndipo alipoamua kufanya maamuzi ya kusema kwa walimu wake wa hapo shuleni lakini walimu wao wakadhani ni kama utani kulingana na maneno ya wanafunzi huyo.
“Alikuwa akiniambia nilale chini halafu ananivua nguo na kujaribu kuingiza uume wake kwangu…lakini nilikuwa naumia .alisema mwanafunzi



Lakini siku moja walimu wa shule hiyo waliamini maneno ya wafunzi huyo baada ya kuonyesha hisia za kuumizwa na kitendo hicho ndipo nao wakaamua kumfikishia taarifa mwalimu mkuu wa shule hiyo ili watafute ufumbuzi wa suala hilo.
 “Sisi walimu tulichokifanya nikwenda kwa mkuu wetu wa shule lengo nikuona mwanafunzi wetu anasaidiwa” walisema walimu
Mwalimu mkuu alisema alichokifanya aliwaita viongozi akiwemo na mwenyekiti wa kamati ya shule ,Mwenyekiti wa kijiji,na wajumbe baadhi wa kamati ya shule ili kuwapa taarifa hiyo.
 “Mimi nilichofanya nilimuuita mwenyekiti wangu wa kamati ya shule na mwenyekiti ya kijiji pamoja na wajumbe wa kamati nikawambia wao wakaamua kwenda na mwanafunzi Hospital pamoja kituo cha polisi lakini baada ya hapo mimi sijuwi kinachoendelea” anasema mwalimu mkuu
Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho amesema ni kweli aliitwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo na akawapa taarifa ya suala hilo lakini walichofanya waliondoka na mtoto pamoja na mtuhumiwa ambaye ndiye Baba mdogo wa mwanafunzi huyo wakaenda Hospital kuchukuwa vipimo na jibu wakapewa kuwa mwanafunzi huyo tayari kashatolewa Bikra.
Aidha amesema baada ya hapo waliongozana hadi kituo cha polisi kilichpo ndani ya kata yao na kuwapa taarifa pamoja na majibu ya vipimo na ndipo mkuu wa upelelezi katika kituo hicho akawambia waliachie jeshi la polisi kazi liweze kufanyia kazi.
“ni kweli niliitwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo na akatupa taarifa ya suala hilo lakini tulichofanya wtuliondoka na mtoto pamoja na mtuhumiwa ambaye ndiye Baba mdogo wa mwanafunzi huyo tukaenda Hospital kuchukuwa vipimo na jibu tukapewa kuwa mwanafunzi huyo tayari kashatolewa Bikra ”
“baada ya hapo tuliongozana hadi kituo cha polisi kilichopo ndani ya kata yetu na kuwapa taarifa pamoja na majibu ya vipimo na ndipo mkuu wa upelelezi katika kituo hicho akatwambia tuliachie jeshi la polisi kazi”
“asaivi sijuwi kinachoendelea maana hata nikiuliza sipata majibu”
Redio mazingira fm tukifika katika kituo cha polisi hicho kilichotajwa lakini majibu tuliyopewa ni kuwa hawana taarifa ya mwanafunzi huyo wala taarifa yeyote kutoka uongozi wa kijiji hicho.
“Sisi hatuna taarifa ya huyo mwanafunzi mliyemtaja na hatujapokea taarifa yeyote kutoka kijiji hicho”
Ikatubidi tumtafute mama mzazi wa mwanafunzi huyo yeye amesema kuwa mwanaye amemusimulia hali ilivyo lakini alipowashirikisha watoto wake wa kiume Kaka zake na Mwanafunzi huyo walichosema ni kwamba waache tu maana mdogo wao yupo hai.
“amemusimulia hali ilivyo lakini nilipowashirikisha watoto wangu wa kiume ambao ni Kaka zake na huyo mwanangu wakaniambia mama achana na mambo hayo maana si mdogo wetu yupo hai kwamba waache tu maana mdogo wao yupo hai”
Taarifa zilipo ni kuwa mwanafunzi huyo amesafirishwa kupelekwa kwa mama yake mzazi kwa madai ya kuwa anaenda likizo lakini taariza tulizozipata kupitia chanzo chetu cha Habari ni kuwa mwanafunzi huyo mipango iliyopo ni kutorudi Shuleni.
Hata hivyo aliyeshiriki kumsafirisha kumpeleka kwa mama yake ni Yule Baba yake mdogo ambaye ndiye anayetuhumiwa kufanya kitendo hicho cha kikatili.

BADO TUNAENDELEA KUFATILIA HADI TUHAKIKISHE SUALA HILI TUNALIKAMILISHA.    

Monday, 4 December 2017

Pesa ya mahindi ya msaada yamludisha Mstaafu ofisini kujibu wilayani Bunda



Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara limetoa siku tano kuanzia leo kwa aliyekuwa afisa kilimo ambaye kwa sasa amestaafu kuhakikisha anatoa taarifa ya kujitosheleza kuhusu uchakachuaji uliofanyika katika pesa ya mahindi ya msaada yalioyogawika ndani ya  halmashauri.

Azimio hilo limetolewa leo katika kikao cha dharura cha kujadili hoja ya mkaguzi wa ndani kutoka mkoani ambapo hoja hiyo emepelekea hadi  kuimbua mambo mengine yaliyokuwa yamejificha ndani.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri Isack Mahela amesema wao kama wawakilishi wa wananchi hawawezi kukaa kimya wakati pesa za wananchi zinatumika sivyo.

Hata hivyo inaelezwa kuwa anayetuhumiwa kuhusuiana na suala hilo la pesa ya mahindi ya msaada kupotea juu juu  afisa huyo ameshasitaafu hivi karibuni.

Awali madiwani wameonekana kutolizishwa na majibu ya wakuu wa idara katika mambo ya msingi yanayohusu halmashauri jambo ambalo wamesema kwa hali hiyo wataisababishia halmashauri hati mbaya.

Saturday, 21 October 2017

Bodi ya filamu tanzania yatuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha muigizaji nguli wa filamu shamila mfikirwa.

Bodi ya Filamu Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Muigizaji nguli Shamila Mfikirwa.
Katika Salamu zake kwa Rais ya Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifamba, Mwenyekiti wa chama cha Waigizaji Ndugu Elia Mjata na wanafamilia wa filamu na uigizaji kwa ujumla Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.
“Kwa niaba ya Bodi nachukua fursa hii kutoa pole nyingi sana kwa familia ya marehemu kutokana na kuondokewa na mpendwa wao, pia Bodi imeguswa na msiba huo na inawaombea wanafamilia kwa Mungu kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu” alisema Bi.Fissoo.
Mwigizaji Shamila Mfikirwa maarufu kama ‘Shamila’ amefariki dunia katika Hospitali ya Occean Road Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2017 alipokuwa akipatiwa matibabu.
Innalilah Wainna Ilayhi Rajiun.
Imetolewa na

Bodi ya Filamu Tanzania.

Wazazi watakiwa kuacha kutuma watoto wao usiku dukani

Zikiwa zimesalia wiki moja wanafunzi wa kidato cha nne nchini kote kuanza mtihani wao wa taifa wazazi na walezi wametakiwa kuwa na desturi ya kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuacha kuwatuma kwenda kununua mahitaji mbalimbali dukani nyakati za usiku kwani kufanya hivyo ni kutoa mwanya kwa watoto hao kukutana na watu wanaoweza kukatisha ndoto zao kwa kuwapatia mimba.
Hayo yamesemwa jana na mgeni rasmi katika mahafari ya 24 katika shule ya sekondari bunda mheshimiwa diwani wa kata ya kabarimu Pastory Ncheye.
Amesema suala la mimba linatokana na wazazi kutowajengea malezi mazuri watoto wao, na kutolea mfano kuwa mzazi anapomtuma mtoto kwenda kufanya biashara usiku au kununua bidhaa usiku dukani inapelekea watoto hao kukutana na watu wanaowashawisha kushiriki nao kufanya ngono hatimae kupata mimba.
Aidha amewatahadharisha wanafunzi kuacha kujihusisha na vitendo vya ngono kwani kupata mimba ni majaliwa lakini watambue kwamba kuna gonjwa hatari la ukimwi.
Mheshimiwa ncheye katika mahafari hayo ameaidi kushirikiana na shule hiyo kurekebisha gari la shule lililoaribika kwa  muda mrefu hivyo kuitaji fedha zaidi ya shilingi milioni moja kukamilika.
Pamoja na hayo pia ncheye ameaidi kuwapelekea miche ya miti ili kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanaendelea kuwa mazuri na ya kupendeza, na kuwasifu kwa jitihada walizozifanya za usafi wa mazingira.
Kwa upande wake mwalim mkuu wa shule hiyo Machota Kora katika risala yake amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya upungufu wa matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa, pamoja na uzio katika mabweni ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Hata hivyo amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika kuwalea watoto kwakuwa wao wenyewe hawawezi na ndiyo maana katika shule hiyo jumla ya wanafunzi watatu waliotakiwa kuhitimu na wanzao walikatisha masomo yao kwa kupata mimba.



Afisa mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa bunda Mkoani Mara bwana Rick steven Kaduri apinga takwimu ya mifugo 770 kufa.

Siku chache baada ya kituo hiki  kuripoti habari kuhusu mifugo zaidi ya 700 kufa kwa tatizo la kukosa maji na majani kwa muda mrefu, hatimae leo mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa bunda Mkoani Mara bwana Rick steven Kaduri amejitokeza na kupinga ukweli wa taarifa hiyo licha ya kukiri kuwa mifugo imekufa.

Amesema kuwa ni kweli mifugo imekufa katika halmashauri ya mji wa bunda, lakini ameshangazwa na idadi iliyotajwa ya mifugo zaidi ya  700 kufa huku akisema kuwa kwa taarifa walizonazo kama halmashauri nzima ni zaidi ya mifugo 1000 imekufa kwa kukoswa maji na majani kwa muda mrefu.
Amesema taarifa kama hizo zilisikika tena guta kuwa zaidi ya ng’ombe 3000 wamekufa lakini bado wanazidi kuzifanyia uchunguzi kubaini ukweli wake.
Amesema tatizo la mifugo kufa imetokana na ukame wa muda mrefu huku akitaja kuwa wafugaji waliokuwa na ng’ombe wenge ndio waathirika wakubwa hivyo amewakumbusha wafugaji kufuga kisasa ili waweza kumudu hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hivi karibuni mtandao huu umewatembelea wafugaji wa kijiji na kata ya rwabu kutaka kujua hali ya mifugo ambapo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Gelad Kuzenza,  alisema kuwa kwa makisio ya chini walikuwa na ng’ombe 1500 na lakini  kwa sasa wamebaki 700 huku akieleza kuwa  bei ya ng’ombe imeshuka hadi shilingi 15,000 huku wanunuzi wakisusia kununua mifugo hiyo wakati mwingine kutokana na hali ya ya kudhoofika zaidi.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafugaji kanda ya ziwa kwa maana ya mikoa ya  Mara, simiyu shinyanga, mwanza geita na Kagera bwana Mrida mshota amekiri kuwepo kwa tatizo la mifugo mingi kufa kwa ukame na hasa ng’ombe ambapo amesema kuwa wameshaanza mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha mashamba ya majani kwa ajili ya mifugo yao.
Amesema zoezi hilo sio la muda mfupi kwa kuwa watanzania wengi na hasa mikoa ya kanda ya ziwa bado wanafuga ng’ombe wa kienyeji na wana mifugo mingi.
Amewataka wafugaji kuanza kubadilika kwa kufuga kisasa ili waweze kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.



Jumla ya wazee 235 katika kata ya neruma wilayani Bunda Mkoani Mara wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu

Jumla ya wazee 235 katika kata ya neruma wilayani Bunda Mkoani Mara  wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu lengo ikiwa ni kuhakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku.

Akisoma taarifa ya utoaji wa huduma za afya na stawi wa jamii Kwa mgeni Rasmi Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya bunda Liberatus Kazana katika maadhimisho ya siku ya wazee Duniani yaliyofanyika Katika kijiji cha Neruma kata ya neruma Oktoba 20 amesema Halmashauri ya wilaya ya Bunda inajumla ya wazee 9,994 waliona miaka 60 na kuendelea.

Kazana Amesema kunachangamoto mbalimbali katika uendeshaji wa huduma za afya na hasa katika kuwahudumia wazee huku gharama za uendeshaji wa huduma za msamaha zimekuwa kubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya hiyo ikitokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji msamaha kama vile akina mama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano,walemavu na wazee.


Kwa upande mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya ya Bunda Masalu Kisasira amesema wao kama serikali wanatambua changamoto hizo hivyo ameahidi kuzifanyia kazi huku akiwasihi wazee kuwa kioo kizuri kwa watoto wao kwa kuwaonya na kuwashauri ili kuwawezesha watoto wao kuwa na misingi bora ya maisha.