Zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni tayari kilo million saba na laki tatu na elfu hamsini na sita tayari zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima wilayani Bunda.
Na Adelinus Banenwa
Zaidi ya tani elfu 7 za pamba tayari zimenunuliwa katika vituo vya AMCOS wilayani Bundahuku ikitajwa asilimia 95 ya pamaba tayari imeshanunuliwa kutoka kwa wakulima.
Hayo yamebainishwa na mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea wakati akizungumza na Mazingira fm ofisini kwake ambapo amesema zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni tayari kilo million saba na laki tatu na elfu hamsini na sita tayari zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima na zoezi linaendelea vizuri.
Ndugu kabea ameongeza kuwa jukumu lililopo kwa sasa ni wakulima wa zao la pamba kung’olea maotea na kuyachoma moto kama ambavyo maelekezo ya kilimo cha zao hilo yanaelekeza.
Katika hatua nyingine kabea ameiambia mazingira fm kuwa tayari maelekezo aliyoyaacha balozi wa pamba Tanzania mhe Aggrey Mwanri ya uanzishwaji wa mashamba darasa yameishaanza kufanyiwa kazi ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda tayari mashamba darasa 385 yameanzishwa huku mashamba darasa 180 kwa halmashauri ya mji wa Bunda.
No comments:
Post a Comment