Mbunge Getere aendelea kukagua shughuli za maendeleo Jimboni - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Tuesday 8 August 2023

Mbunge Getere aendelea kukagua shughuli za maendeleo Jimboni

Mbunge wa Bunda Mhe. Boniface Mwita Getere ameendelea na ziara  kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo. 
Utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Hunyari kata ya Hunyari ambao umetengewa zaidi ya shilingi milioni 800. Umeanza kujengwa mwezi Machi 2023 na unataegemea kukamilika Agosti 2023

Ujenzi wa Vyumba vitano (5) vya madarasa shule ya msingi Hunyari vyenye thamani ya shilingi milioni 100.


Ujenzi wa barabara ya Nyamatutu hadi Manangasi kiwango cha moramu yenye thamani ya shilingi milioni 74


Na Edward Lucas.

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mhe. Boniphace Mwita Getere ameendelea na ziara ya kukagua shughuli za miradi ya maendeleo ndani ya jimbo hilo na kufanya mikutano na wananchi kwa kuwakutanisha na mamlaka husika ili kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miaradi na kujibu hoja za wananchi.

Katika ziara alioifanya jana tarehe 7 Agosti 2023 alitembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Hunyari ikiwa ni pamoja na mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni mia nane ishirini (820, 000,000) unaotekelezwa katika kijiji cha Hunyari ambao ulianza mwezi Machi 2023 na unategemea kukamilika mwezi Agost 2023.

Mhe. Getere alitembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Hunyari ambao umekamilika kwa gharama ya shilingi milioni mia moja (100, 000, 000) na ujenzi wa barabara ya Nyamatutu hadi Manangasi kwa kiwango cha moramu yenye thamani ya shilingi milioni sabini na nne (74,000,000)

Aidha Mhe. Getere alihitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano na wananchi wa Hunyari katika viwanja vya shule ya msingi Hunyari ambapo katika mkutano huo aliambatana na viongozi kutoka idara na taasisi kama TARURA, RUWASA, TANESCO na ELIMU kwa lengo la kujibu hoja za wananchi na kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi katika eneo hilo.
No comments:

Post a Comment