Salama waibuka mshindi wa tatu Kombe la Samia Jimbo la Bunda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 10 August 2023

Salama waibuka mshindi wa tatu Kombe la Samia Jimbo la Bunda

 

Kaptaini wa timu ya Salama akipokea zawadi ya mshindi wa tatu kutoka kwa Mhe. Getere

Timu ya Salama wameibuka mshindi wa tatu katika Kombe la Samia 2023 Jimbo la Bunda kwa kuiburuza timu ya Hunyari goli 3-0 katika viwanja vya shule ya msingi Sarawe.


Magoli ya Salama yamefungwa na John Heziron dakika ya 44' kipindi cha kwanza yakifuatiwa na magoli ya Hemedi Charles na Sanai George dakika ya 60' na 87' kipindi cha pili.


Katika michuano hiyo iliyoratibiwa na Mbunga wa Jimbo la Bunda, Mhe. Boniphace Mwita Getere ilihusisha jumla ya timu 7 kutoka katika Kata zote zinazounda jimbo hilo.


Akitoa zawadi kwa mshindi wa tatu, Mhe. Getere amewaasa vijana kuimarisha urafiki, amani na mshikamano kupitia michezo na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta vurugu na kuwagawa.

Kaptaini wa timu ya Salama akiwa ameshika kiasi cha shilingi 250,000 kama sehemu ya zawadi kwa mshindi wa tatu 

Zawadi kwa mshindi wa tatu ni Jezi, mpira wa miguu na fedha shilingi 250,000.


Fainali itakuwa leo tarehe 10 Agosti 2023 majira ya 10:00 jioni katika viwanja vya Mugeta kati ya Timu ya Mugeta na KetareNo comments:

Post a Comment