Taasisis ya bonde la ziwa Victoria inayohudumia nchi zote ndani ya Afrika Mashariki tayari imeandaa mpango wa kusimika mitambo ya mawasiliano ziwani yenye thamani ya shilingi bilioni 60 pesa ya kitanzania itakayosaidia kutoa taarifa kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa watu wanaotumia ziwa hilo kwa shughuri mbalimbali.
Na Adelinus Banenwa
Zaidi ya watu 1000 hadi 5000 hupoteza maisha kwa kuzama ziwa Victoria kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa vifaa vya uokozi na mawasiliano.
Hayo yamesemwa na Dkt Masinde Bwire kutoka taasisi ya bonde la ziwa Victoria yenye makao yake makuu jijini Kisumu nchini Kenya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi rambirambi kutoka kwenye taasisi hiyo kwa familia zilizopoteza wapendwa wao 14 waliozama ziwa Victoria eneo la Mchigondo kata ya Igundu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara Dkt Bwire amesema kama taasisi tayari wameshaandaa mpango makati wa namna ya kupunguza changamoto ya watu kupoteza maisha ndani ya ziwa.
Akibainisha mikakati hiyo Dkt Bwire amesema kama taasisis ya bonde la ziwa Victoria inayohudumia nchi zote ndani ya Afrika Mashariki tayari imeandaa mpango wa kusimika mitambo ya mawasiliano ziwani yenye thamani ya shilingi bilioni 60 pesa ya kitanzania itakayosaidia kutoa taarifa kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa watu wanaotumia ziwa hilo kwa shughuri mbalimbali kama uvuvi, usafiri n.k.
Aidha ameongeza kuwa pia taasisis hiyo inakwenda kutekeleza mpango wa ujenzi wa vituo vya uokozia katika maeneo yanayozunguka ziwa Victoria ambapo kituo kikuu cha kikanda kitajengwa mkoani Mwanza pamoja na vituo vingine vidogo vidoga katika maeneo mengine ikiwemo Musoma ikiwa na lengo la kutoa msaada wa haraka pindi janga linapotokea ziwani.
Kwa upande wao wakazi wa kitongoji cha Bulomba kata ya Igundu waishukuru serikali na viongozi wilayani Bunda ikiwa ni pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda ambayo ilikuwa pamoja nao tangu tukio la watu kuzama hadi mtu wa mwisho alipopatikana pia wamelishukuru jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kujitoa katika kipindi chote cha kuwatafuta ndugu zao waliokuwa wamezama.
Aidha wakazi hao wamesema mpango wa kuleta mawasiliano imara ziwani na vituo vya uokoaji utasaidia kwa kiwanbgo kikubwa kuondoa vifo vinavyotokana na watu kuzama majini na kukosa msaada.
No comments:
Post a Comment