Wakulima kutumia teknolojia ili kukuza kilimo kama vile kujua ukubwa wa mashamba yao.
Na Adelinus Banenwa
Akifungua kikao kilichowakutanisha wataalam wa halmashauri zote mbili za wilaya ya Bunda katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewataka wakulima kutumia teknolojia ili kukuza kilimo kama vile kujua ukubwa wa mashamba yao.
Mtelela ameyasema hayo katika kikao cha balozi wa pamba nchini Tanzania AggreyMwanri ambapo amefika Bunda kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima namna ya kuandaa mashamba darasa.Picha na Adelinus Banenwa
Balozi Aggrey Mwanri amewataka wakulima wa zao la Pamba wilayani Bunda kuachana na kipimo Cha sentimeter 90 kwa 40 kwa kuwa vipimo hivyo vimepitwa na wakati.
Balozi Mwanri amesema wakulima hawapati mazao tarajiwa kwa sababu hawafuati utaratibu wa kilimo bora cha zao la pamba.
Amesema changamoto kubwa ni wakulima kutopanda pamba kwa mstari kwa kufuata vipimo vya centemeter 60 kwa 30 pili ni kuchanganya zao la Pamba na mazao Mengine na suala maotea.
Akizungumzia kushuka kwa bei ya pamba nchini balozi Mwanri amesema hii imetokana na bei ya soko ya kidunia huku akiwakumbusha wakulima kuwa serikali haipangi bei ya pamba bali inaweka ukomo wa bei ili kumlinda mkulima.
No comments:
Post a Comment