Wenye ulemavu na wanahabari wakutanishwa elimu kupinga ukatili Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday 4 August 2023

Wenye ulemavu na wanahabari wakutanishwa elimu kupinga ukatili Mara

Dismas Ijagara  mkuu wa Division ya maendeleo ya Jamii wilaya ya Butiama, Picha na Adelinus Banenwa

Dismas amewataka watu wenye ulemavu hasa wanawake na wasichana kujiona watu wa kawaida katika Jamii.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa waandishi wa habari kuelimisha Jamii juu ya madhara yatokanayo ya ukatili wa kijinsia katika Jamii hasa kwa kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya siku moja iliyofanyika Kyabari wilayani Butiama mkoani Mara Mgeni rasmi Dismas Ijagara mkuu wa Division ya maendeleo ya Jamii wilaya ya Butiama amesema serikali inashirikiana vyema na Asasi za kiraia katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika Jamii zetu.

Washiriki wa Warsha ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wenye walemavu

Aidha Ndugu Dismas amewataka watu wenye ulemavu hasa wanawake na wasichana kujiona watu wa kawaida katika Jamii.

Mafunzo haya yamewakutanisha vyama vya wenye ulemavu wilayani Butiama na waandishi wa habari chini ya shirika la C.SEMA na UNFPA kwa ufadhili wa Ubalozi wa Finland chini ya mradi wa “Chaguo langu Haki yangu”.


Mkuu wa  miradi  na Mkurugenzi wa huduma simu kwa mtoto kutoka shirika la C.SEMA Michael Marwa,  Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa  miradi  na Mkurugenzi wa huduma simu kwa mtoto kutoka shirika la C.SEMA Michael Marwa amesema Lengo kuu la kuwakutanisha vyama vya wenye ulemavu na wanahabari ni kutaka kujenga ulelewa wa pamoja na kutoka na mpango mkakati wa nini cha kufanya kila mtu kwa nafasi yake Ili kuondokana na ukatili huu kwa wanawake na wasichana hasa wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment